Steve Mweusi
Steve Moses Musa | |
---|---|
| |
Maelezo ya awali | |
Pia anajulikana kama | Steve Mweusi |
Amezaliwa | 16 Septemba 1990 |
Asili yake | Mkoa wa Katavi, Tanzania |
Kazi yake | muigizaji, vichekesho |
Steve Moses Musa (anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Steve Mweusi; amezaliwa Majengo, wilaya ya Mpanda, Mkoa wa Katavi, 16 Septemba 1990) ni muigizaji wa vichekesho vifupi ambavyo hutazamwa zaidi katika mtandao ya kijamii [1]. Sanaa yake ambayo alikuja kuianza rasmi jijini Dar es Salaam mnamo mwaka 2018 iliweza kufungua ndoto zake za kuwa mmoja wa wasanii maarufu wa uigizaji wa vichekesho nchini Tanzania.
Maisha ya awali
[hariri | hariri chanzo]Steve Mweusi ameweza kuhitimu masomo ya shule ya msingi nduwi iliyopo katika wilaya ya mpanda. Amekuwa rasmi kwenye sanaa hii ya uchekeshaji kwa miaka zaidi ya minne (4) na wakati hapo awali alikuwa amejiajiri kwenye shughuli ya kusafisha mazingira maeneo ya kariakoo jijini Dar es salaam kabla hata ya nyota yake kuweza kujulikana na watanzania wengi zaidi.
Maisha yake ndani ya sanaa
[hariri | hariri chanzo]Kutokana na yeye kupenda sanaa kipindi wakati aikiwa mdogo na wakati yupo masomoni, Steve Moses Musa aliweza kuendeleza sanaa hiyo zaidi kwa upande wa uchekeshaji mpaka pale uwezo wake ulipoweza kufikia hatua ya kujulikana na watanzania wengi zaidi hadi kufanya video yake ambayo aliifanya Novemba 14 mwaka 2018 kuweza kupata watazamaji waliofikia takribani milioni kumi na sita katika mtandao wa Youtube.[2][3][4]
Kwa hatua hii mchekeshaji Steve Moses Musa au ajulikanaye kwa jina la kisanii kama Steven mweusi hatua hiyo ilimfanya kupata nguvu zaidi na hamasa ya kuweza kuendeleza kipaji chake cha uchekeshaji nchini Tanzania na kuendelea kutoa video zake mbalimbali za uchekeshaji ambazo ziliwafikia watu wengi na kuzidi kujulikana.
Msanii Steve mweusi alikuja kuungana na kijana mdogo aitwaye Selemani Omary Manjaka au kwa jina la kisanii Dogo Sele ambaye mpaka sasa anafanya naye kazi ya sanaa ya uigizaji kwa juhudi hizo ziliweza kufikia hatua ya kumfanya kijana huyu mwenye umri mdogo ambaye kipaji chake kilikuja kuonekana na Steve mweusi na kuweza kukipeleka kipaji chake cha sanaa ya uchekeshaji hadi kuweza kupata nafasi ya kupanda kwenye jukwaa la kufanya stand up comedy liitwalo Cheka tu.[5]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Steve Mweusi - YouTube". www.youtube.com. Iliwekwa mnamo 2023-04-27.
- ↑ Steve mweusi (Mwizi), iliwekwa mnamo 2023-04-27
- ↑ "Hii ndio video ya kwanza Tanzania kufikisha views Milioni 16 kwa wiki kwenye mtandao wa YouTube, utashangaa msanii mwenyewe – Bongo5.com". bongo5.com. Iliwekwa mnamo 2023-04-27.
- ↑ "Hii ndio video ya kwanza Tanzania kufikisha views Milioni 16 kwa wiki kwenye mtandao wa YouTube, utashangaa msanii mwenyewe". UDAKU SPECIAL. Iliwekwa mnamo 2023-04-27.
- ↑ DOGO SELE KWENYE WEEKLY EDITION, iliwekwa mnamo 2023-04-27