Nenda kwa yaliyomo

Sogdia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya enepo la Sogdia ya kihistoria

Sogdia au Sogdiana (Gir. Σογδιανή) ilikuwa eneo la kihistoria katika Asia ya Kati ng'ambo ya mto Oxus, milima ya Altai inapoanza. Eneo lake leo hii limegawanywa kati ya nchi za Uzbekistan na Tajikistan. Tajikistan huwa hadi leo na mkoa wa Sughd (Суғд).

Zamani za kabla ya Kristo kuzaliwa mara nyingi iliunganishwa na Baktria. Kati ya miji yake muhimu kuna Samarkand na Bukhara. Katika karne kabla ya Kristo ilikaliwa na Wasogdia waliotumia lugha iliyokuwa karibu na Kiajemi na Sogdia ilikuwa jimbo la milki ya Uajemi.

Baadaye makabila ya Waturki waliingia hadi lugha zao ziliipata kipaumbele hadi leo.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]