Nenda kwa yaliyomo

Snorri Sturluson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Snorri Sturluson (kwa Kiiceland Snorri mwana wa Sturla; 1178 - 22 Septemba 1241) alikuwa mshairi, mwandishi wa historia na kiongozi wa kisiasa nchini Iceland.

Anajulikana hasa kama mtungaji wa kitabu cha Edda kinachokusanya habari za utamaduni na dini ya Iceland ya kale kabla ya kufika kwa Ukristo pamoja na kanuni kwa kazi ya mshairi na mwimbaji wa mashairi yanayosimulia historia ya taifa.

Aliandika pia historia ya wafalme wa Norwei.

Mwenyewe alipokea mafunzo ya kuandika na kusoma, pia lugha ya Kilatini, elimu ya dini ya Kikristo na sheria ya Kiiceland. Wazazi walimkabidhi kwa chifu mkubwa aliyemlea kijana.

Alichaguliwa baadaye mara mbili kama msimamizi wa Althing iliyokuwa bunge la Iceland.

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Snorri Sturluson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.