Nenda kwa yaliyomo

Simone Gbagbo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Simone Gbagbo

Simone Gbagbo in 2006

Mke wa aliyekuwa raisi wa Ivory Coast
Muda wa Utawala
26 October 2000 – 11 April 2011
mtangulizi Rose Doudou Guéï
aliyemfuata Dominique Folloroux-Ouattara

tarehe ya kuzaliwa 20 Juni 1949 (1949-06-20) (umri 75)
Moossou, Grand-Bassam, French West Africa
chama Ivorian Popular Front
ndoa Laurent Gbagbo
watoto 5

Simone Ehivet Gbagbo (alizaliwa 20 Juni 1949)[1] ni mwanasiasa wa Ivory Coast. Yeye ni rais wa kundi la wabunge la Ivorian Popular Front (FPI) na ni makamu wa rais wa FPI. Kama mke wa Laurent Gbagbo, rais wa Côte d'Ivoire kuanzia 2000 hadi 2011, pia alikuwa mke wa rais wa Ivory Coast kabla ya kukamatwa kwao na vikosi vinavyomuunga mkono Ouattara.

Alizaliwa mnamo 1949 huko Moossou, Grand-Bassam akipewa jina la Simone Ehivet, binti wa Jean Ehivet, afisa wa polisi wa eneo hilo, na Marie Djaha, Simone Gbagbo alisomea historia na kutunukiwa udaktari katika fasihi simulizi. Alifanya kazi katika taaluma ya isimu kama kiongozi wa chama cha wafanyakazi wa Ki-Marxist na alipewa jina la utani katika vyombo vya habari vya Ivory Coast kama "Hillary Clinton des tropiques".

Mama wa mabinti watano, wa mwisho wawili akiwapata akiwa na mume wake wa sasa, Laurent Gbagbo,[2] alishiriki katika vuguvugu la mgomo wa walimu wa 1982. Simone na Laurent Gbagbo, kabla ya ndoa yao, walianzisha kikundi cha kisiasa cha siri ambacho baadaye kilijulikana kama FPI. Alikuwa mpiganaji katika kundi la trades union katika miaka ya 1970, alifungwa gerezani mara kadhaa wakati wa mapambano ya uchaguzi wa vyama vingi.

Kufuatia kuanzishwa kwa uchaguzi wa vyama vingi, Gbagbo na mumewe walikamatwa kwa madai ya kuchochea ghasia Februari 1992 na kukaa jela kwa miezi sita. Mnamo 1996, alikua naibu wa FPI kutoka Abobo (sehemu ya Abidjan) katika Bunge la Kitaifa la nchini humi. Mnamo 1998, alikua mkristo mwinjilisti(aliokoka) baada ya kunusurika kwenye ajali ya gari.[3][4]

Alichaguliwa tena katika bunge la kitaifa kama naibu wa FPI kutoka Abobo katika uchaguzi wa wabunge wa Desemba 2000,[1] Gbagbo pia ni Rais wa Kundi la Wabunge la FPI.[5] Katika kongamano la tatu la kipekee la FPI, lililofanyika kuanzia tarehe 20 hadi 22 Julai 2001,[6] Alichaguliwa kuwa makamu wa pili wa rais wa FPI.[7]

  1. 1.0 1.1 "National Assembly website". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-12-19. {{cite web}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help), National Assembly website (2007 archive page) .
  2. "Soir Info : Votre quotidien nocturne !". Soir Info.
  3. AFP, Côte d’Ivoire : l’influente Simone "Maman" Gbagbo libérée après 7 ans de prison, sudouest.fr, France, Aug 9, 2018
  4. Cheikh Yerim Seck, "La vraie Simone Gbagbo", Jeune Afrique, 10 December 2006.
  5. "Simone Ehivet Gbagbo", Jeune Afrique, 23 December 2007 .
  6. Tidiane Dioh, "Le FPI en ordre de bataille", Jeuneafrique.com, 31 July 2001 .
  7. List of members of the FPI Secretariat-General Archived 29 Juni 2008 at the Wayback Machine., FPI.ci, .