Shule ya Strathmore
Shule ya Strathmore ni shule ya kwanza ya Kenya ambayo haikuwa na ubaguzi wa rangi iliyoanzishwa mwaka wa 1961 katika eneo la Lavington wilayani Nairobi. Mwanzoni, ilikuwa chuo ambacho elimu yake ilikuwa inafika hadi kidato cha sita na mfumo wa elimu ulikuwa wa Kiingereza (kozi za kiwango cha A ndizo zilizokuwa zinafunzwa wakati huo) na mwaka wa 1963 ilibadilisha bodi yake ya kuwatahini wanafunzi kutoka Cambridge School Certificate Examination hadi London GCE Mwaka wa 1977 ikawa shule ya upili kikamilifu. Mwaka wa 1988, shule hiyo ilianza kutoa elimu ya KCSE - Kenya Certificate of Secondary Education - mitaala ambayo ifuatavyo hadi sasa. Kundi la kwanza la wanafunzi wa shule ya Msingi (wanafunzi wa miaka 6-7) waliingia mwaka wa 1987. Kwa sasa haina wanafunzi wowte wanaolala bwenini.
'The Scroll', gazeti la shule, ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1963. Toleo la mwisho lilichapishwa mwaka wa 2006 ndiposa kuiachia njia teknolojia mpya ya aina ya DVD iitwayo ‘The Scroll Digital’ (maarufu kama 'digital').
Kila mwaka shule hii huwatuza wanafunzi wawili bora wanaohitimu. Mmoja akiwa Mwanaspoti wa Mwaka, na mwingine akiwa Msomi wa Mwaka. Wale ambao hutuzwa majina yao huandikwa katika 'Honours Board' shuleni. Pia kuna bodi ya heshima kwa Msomi wa Mwaka kutoka kwa Shule ya Msingi.
Tangu mwaka wa 1961 ni mtu mmoja tu ambaye amepata tuzo zote mbili: James McFie mwaka wa 1963.
Shule ya Strathmore inasifa nzuri ya kuwa moja kati ya shule chache (kama siyo ya kipekee) nchini Kenya ambayo haina viranja. Wanafunzi wana uhuru na wanatarajiwa kuwajibika na uhuru huo.
Shule hii hana majumba. Wanafunzi huwateua viongozi wa darasa (Manahodha na Manaibu wa Nahodha) ambao huchagua wanafunzi wenzao katika timu zao (Ndovu, Nyati, Chui na Simba). ). Hii inafanywa katika kila darasa na hakuna uhusiano na matimu katika madarasa mengine (hivyo hakuna mfumo wa jumba) kwani kila timu inafanya kazi yake kibinafsi.
Kuna mkondo mbili katika upande wa shule ya upili, A na ALPHA. Mkondo zote mbili ni wapinzani wakuu kwani wanachama wa kila mkondo hukumbuka majumba yao hata miaka kadhaa baada ya kuhitimu kutoka kwa shule. Ni kawaida sana kusikia kauli kama 'jamaa huyo ni mbaya zaidi kuliko mtu wa Alpha' au 'ugonjwa huo ni mbaya kama vile virusi A' katika mazungumzo miongoni mwa wanafunzi waliohitimu.
Shule hii ina timu za michezo, kila timu ikiwa na jina lake la kibinafsi na historia yake ya kibinafsi. Timu ya raga, maarufu kama “The Bandits”, ndiyo timu maarufu kwa michezo yote shuleni. Mwaka jana walikuwa washindi wa tamasha ya Blackrock ya Shule ya St Mary, tamasha ya raga kubwa zaidi ya shule nchini Kenya. Wao huvaa mashati ya yenye rangi nyeusi, samawati na nyeupe.
Timu zingine ni “Pirates” (timu ya mpira wa kikapu) na “Stallions” (timu ya voliboli) ambayo ilishinda ligi ya mkoa wa Nairobi mara kadhaa katika miaka ya 1970. Timu ya kriketi inajulikana kama “Stalwarts”.
Wapinzani wao wakuu wa Michezo Shule ya St Mary ya Nairobi, majirani wa karibu na wanamichezo maashuhuri nchini Kenya. Wanafunzi wa Strathmore mara nyingi huwaita 'kijiji katika ng’ambo ile ya mto' kwani shule hizi mbili zinagawanywa mpakani na Mto wa Nairobi.
Mafundisho ya ukweli na malezi ya kidini katika Shule ya Strathmore imekabidhiwa Opus Dei, a sehemu ya Kanisa Katoliki.
Shule ya Strathmore ilikuwa katika nafasi ya pili katika orodha ya shule bora zaidi nchini Kenya kutokana na msingi wa mwaka wa 2006 wa Kenya Certificate of Secondary Education.
Wanafunzi mashuhuri
[hariri | hariri chanzo]- Michael Wamalwa Kijana (Aliyekuwa Makamu wa Rais)
- Askofu Anthony Muheria (Askofu Katoliki wa Jimbo la Kitui)
- David Mathenge aka Nameless (mwanamuziki)
- Gideon Moi