Nameless

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka David Mathenge)
Jump to navigation Jump to search

David Mathenge (amezaliwa Agosti 1976), anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii Nameless, ni msanii wa kapuka nchini Kenya.

Taawasifu[hariri | hariri chanzo]

Yeye alipata umaarufu mwaka 1999 kupitia Ushindani wa "Star search" uliofanywa na stesheni ya radio ya [Capital(98.4 fm) http://www.capitalfm.co.ke], ambayo alishinda kwa wimbo wake wa awali "Megarider" Wimbo huu unaongelea m kijana ambaye hana pesa na ilhali anajaribu kumpata kipusa.Fedha alizonazo zinatosha tu tiketi ya Kenya Bus , na si maisha ambayo msichana huyo anataka. Alifanya wimbo huo na na mtayarishaji Tedd Josiah na ulikaa kwenya kwenye chati kwa wiki kadhaa Alitia saini na Ogopa Deejays mnamo mwaka wa 2001.katika Ogopa DJ's alikuwa pamoja na wasanii kama vile marehemu E-Sir amabaye walifanya wimbo wa "Boomba Train," na Amani : "Ninanoki" mwaka wa 2002 wimbo ambao ulivunja rekodi kwenya chati nchini Kenya kwa kusalia siku 110 nambari moja

Amekwenda kwenye ziara kaadhaa Afrika Mashariki , Marekani na pia Uingereza Alitoa albamu yake ya "on fire mwaka wa"2004. Pia mwaka huo huo wa 2004 Mathenge alimuoa msanii mwenzake Wahu Kagwe waliyekuwa wakirekodi pamoja katika Ogopa DJ's. Wana mtoto mmoja, binti ambaye alizaliwa mwaka 2006. Yeye pia ni mbunifu na alfuzu kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.

Kikundi cha 'pop' kutoka Afrika Kusini ; Jamali walitoa wimbon wimbo wa "nigger" na ilisemekana kwamba waliuiba wimbo huo kutoka kwa Nameless. Lakini baadaye Jamali walikubali kumshirikisha Nameless kama Mwandishi wa "maisha" kwenye albamu yao ya "Yours Fatally"

Yeye alikuwa miongoni mwa orodha ya watu mia moja (100) wenya ushawishi mkubwa sana nchini Kenya kama iliyotolewa na gazeti la The Standard Agosti 2007 [1][2]

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

Kuchaguliwa[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viunganish vya nje[hariri | hariri chanzo]