Nenda kwa yaliyomo

Shekhinah (mwimbaji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwanamuziki Shekhinah

Shekhinah Thandi Donnell (alizaliwa 2 Oktoba, 1994), anajulikana kwa jina moja kama Shekhinah, ni mwimbaji na mtunzi wa nyimbo kutoka Durban, Afrika Kusini . Shekhinah alikuwa miongoni mwa washindi 32 bora wa msimu wa 7 wa mashindano ya SA Idols mwaka 2011 na miongoni mwa washindi 6 bora wa msimu wa 8 wa SA Idols mwaka 2012. [1]

Albamu yake ya kwanza ya Rose Gold ilitolewa mnamo Oktoba 2017 na kuthibitishwa kuwa na hadhi ya platinamu na RiSA manamo 31 Agosti 2018. [2] [3] [4] Rose Gold ilitoa nyimbo tatu za nambari moja zilizojulikana kama "Suited"; "Please Mr." na "Different".

Albamu yake ya pili ya Trouble In Paradise, ilitolewa Mei 2021.

2016-2018: Rose Gold (2018)

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka 2017, Shekinah alitoa wimbo wake wa kwanza "Suited", ambao ulishika nafasi ya 1 kwenye chati za muziki za Afrika Kusini na kuthibitishwa kwa plaque ya hadhi ya almasi na tasnia ya kurekodi ya Afrika Kusini (RiSA). [5] Mnamo 2018, "Please Mr" na "Different" zilitolewa mwaka huo huo, "Please Mr" iliidhinishwa na plaque ya hadhi ya dhahabu. [6]

Mnamo Oktoba 6, 2017, albamu yake ya kwanza ya Rose Gold ilitolewa nchini Afrika Kusini na Sony Music Entertainment Africa.

Mnamo Mei 7, 2021, albamu yake ya pili ya Trouble In Paradise ilitolewa nchini Afrika Kusini. [7] [8]

  1. "Shekhinah Donnell rises above the stars : AFDA". www.afda.co.za (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-08-03. Iliwekwa mnamo 2017-08-03.
  2. Makhudu, Tshegofatso. "Shekhinah goes gold and platinum". channel24. Iliwekwa mnamo 26 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Shekhinah's Rose Gold goes gold". BONA Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-07-29. Iliwekwa mnamo 26 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Shekhinah's Rose Gold Album Attain Gold Status". samusicmag. Iliwekwa mnamo 26 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Shekhinah's Hit Single 'Suited' Has Been Certified Platinum". okayafrica. Iliwekwa mnamo 26 Januari 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Shekhinah's "Please Mr" Goes Gold". Fakaza. Fakaza News. Iliwekwa mnamo 8 Mei 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Shabangu, Nobantu (7 Mei 2021). "Shekhinah Experiences 'Trouble in Paradise' on Her Latest Album - OkayAfrica". OkayAfrica.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. Reporter, Entertainment (Novemba 20, 2020). "Shekhinah delays 'Trouble In Paradise' album release". Independent Online.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shekhinah (mwimbaji) kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.