Schiphol
Mandhari
Schiphol ni uwanja wa ndege wa kimataifa wa Amsterdam nchini Uholanzi. Ni kati ya nyanja za ndege kubwa duniani ukiwa na abiria zaidi ya milioni 46 wanaopita humo na hii ni nafasi ya nne ya Ulaya na nafasi ya 12 duniani.
Jina kamili kwa Kiholanzi ni Luchthaven Schiphol au kwa Kiingereza Amsterdam Airport Schiphol. Kifupi chake ni AMS.
Ni kituo kikuu cha KLM.
Uwanja huu upo kilomita 17.5 kusini kwa Amsterdam na safari kwa treni kutoka mjini ni dakika 20.