Nenda kwa yaliyomo

Sayansi ya jamii

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Sayansi za jamii)
Miingiliano ya kijamii na matokeo yake huchambuliwa katika sayansi ya jamii.

Sayansi ya jamii ni somo kuhusu jamii za binadamu. Ni sayansi ya kijamii ambayo hutumia mbinu mbalimbali za uchunguzi kwa kupima ili kutengeneza na kusafisha mwili wa maarifa na nadharia kuhusu shughuli za kijamii za binadamu. Mara nyingi huwa na lengo la kuyatumia maarifa hayo ili kuisaidia jamii. Mada mbalimbali katika sayansi ya kijamii ni kama vile eneo dogo la kiwakala na mwingiliano hadi eneo kubwa la mifumo na miundo ya kijamii.

Sayansi ya jamii ni taaluma pana sana ukitazama mbinu inayotumia na mada inazolenga. Taaluma zake za kijadi zimekuwa ni mpango wa jamii (yaani, uhusiano wa watu wa madaraja mbalimbali katika jamii), dini, kuenezwa kwa dhana za kidunia, usasa, utamaduni, na mitazamo yake imehusisha mbinu za utafiti za idadi kubwa na za ubora. Kwa sababu mengi ambayo sisi binadamu hufanya huweza kujumuisha chini ya mpangilio wa kijamii, sayansi ya jamii imezidi kupanua mathumuni yake hadi kwa taaluma zingine kama zile za matibabu, ujeshi na ya taasisi za kuadhibu, mtandao, na hata umuhimu wa matendo ya kijamii katika kuendelea kwa maarifa ya kisayansi.

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sayansi ya jamii kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.