Samuel Kwesi Oppong

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Samuel Kwesi Oppong (Alifariki mnamo tarehe 3 Desemba, 2001), alijulikana sana katika tasnia ya uigizaji na miongoni mwa mashabiki kama "S.K. Oppong" alikuwa mwigizaji wa Ghana, mwanamuziki na msimuliaji hadithi. Oppong alidumisha alama zake za biashara ambazo zilimtofautisha na waigizaji wenzake. Kando na uigizaji, pia alikuwa mpiga gitaa na kiongozi wa bendi na amekuwa katika biashara ya muziki tangu miaka ya 1950. Alitunga, kuimba na kurekodi nyimbo kadhaa wakati wake kama mwanamuziki wa kitaalamu. Alianzisha Bendi ya Gitaa ya SK Oppong iliyozunguka nchi nzima na kupiga katika baadhi ya kumbi maarufu. Kundi hili lilipata mafanikio ya hali ya juu kwenye tasnia ya muziki ya Ghana kuanzia mwaka wa 1959 na nyimbo kama vile "Obaa Kunadu", "Akwankwaa Hiani", "Kyere Me Ade a Meye", miongoni mwa nyimbo zingine[1].

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Mashuhuri S. K. Oppong alifariki katika Hospitali ya Kufundisha ya Korle-Bu mnamo tarehe 3 Desemba 2001, baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa ambao haukujulikana, akiwa na umri wa miaka 55. Waziri wa Habari na Masuala ya Rais wa Ghana wakati huo, Bw Jake Obetsebi-Lamptey alimwelezea SK Oppong kama "mfano wa kuigwa aliyeelimisha Waghana kupitia sanaa[2]. Alizikwa rasmi tarehe 1 Februari ambapo maelfu ya wenzake kutoka Ofoso Dadzie, tasnia ya filamu, na mashabiki walitoa heshima zao za mwisho. Oppong alizikwa siku iliyofuata kwenye  Makaburi ya Osu[3].

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Alikuwa mwanamuziki mahiri na kiongozi wa kikundi cha maigizo cha Osofo Dadzie.  Alitunga nyimbo nyingi za hali ya juu[4].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Government informed about S.K.Oppong's death (30 November 2001).
  2. https://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/NewsArchive/Government-informed-about-S-K-Oppong-s-death-20872
  3. https://www.ghanaweb.com/GhanaHomePage/NewsArchive/Government-informed-about-S-K-Oppong-s-death-20872
  4. http://www.fagostore.com/vare/3120-sk-oppong-abusua-bcne-special-lp