Salim Kikeke

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Salim Kikeke
Nchi Tanzania
Kazi yake Mtangazaji wa BBC

Salim Kikeke ni Mtanzania mwandishi wa habari na mtangazaji wa televisheni anayefanya kazi kwa sasa katika shirika la habari la BBC. Anasimamia kipindi cha "Focus on Africa" kwenye BBC World News, "Amka na BBC" na "Dira ya Dunia" kwenye BBC News Swahili katika BBC World Service.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Kazi ya kwanza ya Kikeke ilikuwa uchimbaji madini nchini Tanzania mwaka 1995, miaka mitatu baada ya kuhitimu. Baadaye, alijiunga na Radio Tanzania kama mwandishi wa miswada, halafu akawa mtayarishaji na mtangazaji wa muziki. Kuanzia mwaka 2000 hadi 2001, alifanya kazi kama mtangazaji katika kituo cha Channel 10 na alitoa matangazo kwa luga ya Kiswahili na Kiingereza.

Kikeke aliingia katika tasnia ya televisheni mwaka 2001 na akafanya kazi kama mtangazaji katika kituo cha ITV, kituo cha televisheni cha Tanzania, hadi mwaka 2003 alipojiunga na BBC kama mtayarishaji na mtangazaji wa kipindi cha redio cha Kiswahili asubuhi kinachoitwa "Amka na BBC" na baadaye alitengeneza na kuwasilisha Dira ya Dunia, jarida la habari la Afrika Mashariki na Kati kwa Kiswahili kwenye BBC News Swahili katika Huduma ya Dunia ya BBC. Kwa sasa, anasimamia kipindi cha Focus on Africa katika BBC World News. Wakati akiwa BBC, Kikeke aliripoti uchaguzi wa Marekani mwaka 2008, Kombe la Dunia la mwaka 2010 nchini Afrika Kusini, shambulio la Westgate mwezi Septemba 2013 nchini Kenya, na mazishi ya aliyekuwa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, pamoja na matukio mengine mengi.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Salim Kikeke kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.