Nenda kwa yaliyomo

Saa (ala)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Saa kwenye kituo cha reli Zurich, Uswisi.
Kwa kizio cha kuhesabu mwendo wa wakati tazama saa

Saa ni kifaa kinachonyesha na kupima mwendo wa wakati. Saa ndogo huvaliwa na watu mkononi au kubebwa mfukoni, saa kubwa huwekwa ukutani au mahali pa juu mjini kwa watu wote kuona. Saa zmo ndani ya mashina na vifaa vingine vyenye kazi ya kutawala miendo yao.

Siku hizi vifaa kama simu ya mkononi hufanya kazi ya kuonyesha wakati pia.

Hii saa ya jua inaonyesha takriban saa mbili na nusu.

Watu wametazama mwendo wa wakati tangu milenia ya miaka na mwanzoni walitegemea mwendo wa jua jinsi inavyoonekana angani. Katika maeneo mbali kidogo na ikweta mwendo huu unaruhusu kutumia kuangalia mwendo wa kivuli kulingana na mwendo wa jua na hapo ni asili ya saa ya jua.

Saa ndogo ya mchanga unaonyesha dakika 5 kwa upishi wa mayai.

Mbinu mwingine ulikuwa chombo ambako ama maji au mchanga unapita kutoka chombo cha juu katika shimo ndogo kwenda chombo cha chini. Kutokana na kiwango wa ujazo wa chombo cha chini wakati hupimwa. Mifano ya kwanza ya saa ya maji inajulikana kutoka Misri. Saa ya mchanga hutumiwa hadi leo kwa mfano kwa kushika muda katika upishi.

Tangu takriban miaka 600 saa zilibuniwa zisizotegemea tena jua au maji lakini hutumia nguvu ya kamani iliyoruhusu kupunguza ukubwa na uzito na kupata saa za kubebwa na mtu mfukoni kila anapoenda.

Katika karne ya 20 mitambo ya umeme iliunganishwa na saa na seiku hizi saa nyingi huendeshwa kwa nguvu ya umeme wa beteri.

Maisha ya kisasa hutegemea saa za elektroniki na saa atomia zinazopima wakati kikamilifu hadi nanosekunde au chini yake.

Saa ya mkono[hariri | hariri chanzo]

Dhana ya saa ya mkono ina historia ndefu toka wakati wa uzalishaji wa saa za mwanzo kabisa katika karne ya 16. Malkia Elizabeth I wa Uingereza alipokea saa ya mkono kutoka kwa Robert Dudley mnamo mwaka wa 1571. Mwaka wa 1775 saa ilipatikana yenye uwezo wa kukaza kamani yake kwa nishati ya msuko suko wa mkono mtu akitembea na mpaka wa leo inatumika na watu wengi. Saa ya mkono ya zamani kabisa iliyopo hadi hivi sasa (iliyokuwa ikiitwa saa ya bangili) ilitengenezwa mwaka 1806. Mwanzoni saa za mkono zilikuwa zikivaliwa na wanawake tu, wakati wanaume walikuwa wakitumia saa za mfukoni hadi karne ya 20.[1]

Tangazo la saa iliyotengenezwa na Mappin & Webb mwaka 1898.

Saa za mkono zilianza kuvaliwa na wanaume wanajeshi mwisho mwa karne ya 19 kwa ajili ya kupanga vyema vita. Kampuni ya Garstin ya London ilipata hati miliki ya "Watch Wristlet" mwaka 1893, lakini walikuwa wakitengeneza saa miundo kama hiyo tangu miaka ya 1880. Maofisa wa Jeshi la Uingereza walianza kutumia saa za mkonononi wakati wa kampeni ya kijeshi ya kikoloni katika miaka ya 1880, kama vile wakati wa Vita ya Anglo-Burma ya 1885.[1] Wakati wa Vita ya kwanza ya Makaburu, umuhimu wa kuratibu harakati za vikosi na kusawazisha mashambulizi dhidi ya Makaburu ulikuwa muhimu sana, na matumizi ya saa za mkono ulianza kuenea miongoni mwa maofisa wa kijeshi. Kampuni ya Mappin & Webb ilianza uzalishaji wa saa za wanajesho wakati huko Sudan mnamo mwaka 1898 na kuongeza kasi ya uzalishaji wakati wa Vita ya Pili ya Makaburu miaka michache baadaye. Katika bara la Ulaya kampuni ya Girard-Perregaux na kampuni nyingine za Uswisi zilianza kutengeneza saa za mkono za maofisa wa jeshi la Ujerumani mwaka 1880.

Kawaida saa ubora wa saa unahusishwa na mambo mbalimbali kama vile saa inavyoweza kuzuia maji. Shirika la Kimataifa la Usanifishaji (kwa kifupi ISO) limetoa vipimo maalum vya saa zinavyozuia maji.

Saa zaweza kugawiwa katika makundi mawili makuu kuzingatia kizazi; saa za zamani (analog) na saa za kisasa/za dijiti ambazo ni za kielektroni.[2]

Pia zinaweza kugawiwa katika makundi saba kulingana na mtindo na utenda kazi:

  • saa za kujiendesha (automatiki) - saa zisizo hitaji betri
  • saa za kronogilafia (chronograph watches) - saa zijulikanazo kwa Kingereza kama "Stop-Watch" za kupimia mda mfupi hasa wakati tendo kama mbio zinafanyika
  • saa zisizo na mengi (minimalist watches) - saa zisizo na marembesho mengi
  • saa za quartz - saa zinazo tumia teknolojia ya quartz
  • saa za kivazi - saa za kisanaa zinazolenga mvuto wa kipeee
  • saa za kifahari - saa zenye bei ghali mno zinazoundwa kwa kulenga matajiri na mara nyingi huendana na vitu vya fahari kama magari na simu
  • saa zinazotumia nishati ya jua

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "The Evolution of the Wristwatch". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-12-08. Iliwekwa mnamo 2018-07-11.
  2. Great Watches NYC (17 Machi 2018). "Digital vs Analog Watch - Which is Better?". Great Watches NYC (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-07-26. Iliwekwa mnamo 10 Julai 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.