Rwekaza Mukandala

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Rwekaza Sympho Mukandala (alizaliwa Bukoba, Tanzania, 30 Septemba, 1953) ni profesa mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Tanzania [1].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Alipata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Bukoba, na elimu ya sekondari katika shule za Tabora na Musoma. Baadae alijiunga na chuo cha Dar es Salaam (1973 - 1976), ambapo alipata Shahada ya Sanaa (Hons.) juu ya Uhusiano wa Kimataifa na Utawala. Mwaka 1977 alitunukiwa shahada ya uzamili ya Utawala wa maendeleo katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwaka 1988 alipata shahada ya uzamivu katika Sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha California, Berkeley, na cheti cha Uchumi katiba mpya. Pia alitunukiwa zawadi ya Peter Odegard kama mwanafunzi bora wa shahada ya uzamivu huko California.

Baada ya kumaliza shahada yake ya uzamivu, alirejea chuo kikuu cha Dar es Salaam mnamo mwaka 1988 kama Mhadhiri mkuu katika sayansi ya siasa na utawala wa Jamii. Tangu hapo mpaka sasa amefanikiwa kutunukiwa nafasi mbalimbali za kitaaluma na kiutawala kama Profesa wa sayansi ya siasa na utawala wa jamii.

Profesa Mukandala hufundisha Kanuni za jumuia (Organization theories), Utawala wa Umma, Demokrasia na Uchaguzi.

Pia ni Mwenyekiti wa taasisi mbalimbali zikiwemo REDET, TEMCO, ESRF, EAFUI.

Katika kipindi cha masomo yake ambapo ameweza kufikia hatua ya kuitw profesa, ameweza kuandika vitabu mbalimbali.

Amehudumu kama makamu mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa takriban miaka kumi; amestaafu mwaka 2018 na nafasi yake imeshikwa na profesa Anangisye

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. www.udsm.ac.tz
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rwekaza Mukandala kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.