Rus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Rus ya Kiev iliyounganisha karibu maeneo yote ya Rus mnamo mwaka 1237 kabla ya kufika kwa Wamongolia.

Rus (Русь kwa Kirusi, Kiukraine na Kibelarus) ni eneo la kihistoria katika Ulaya ya Mashariki iliyokaliwa hasa na wasemaji wa lugha za Kislavoni likitawaliwa na familia zenye asili ya Skandinavia.

Watu walioitwa Warus walitokea Skandinavia na kufanya biashara katika Ulaya ya Mashariki kati ya Bahari ya Baltiki na Bahari Nyeusi hadi Mediteranea wakitumia mito kama njia. Walianzisha miji kadhaa wakafaulu kuunganisha au kutawala makabila ya Waslavi walioishi katika maeneo hayo[1]. Waliunda milki kadhaa zilizostawi kuanzia karne ya 9 hadi kuja kwa Wamongolia katika karne ya 13.

Milki kubwa zaidi ilikuwa Rus ya Kiev na mtawala wake aliamua kupokea Ukristo wa Kiorthodoksi mnamo mwaka 988[2]. Katika karne ya 11 milki mbalimbali ndani ya Rus zilianza kupigana kati yao. Baada ya uvamizi wa Wamongolia, Kiev iliharibika kabisa lakini mtawala wa jimbo kwenye mashariki alibaki akaanzisha utemi wa Moscow ulioendelea na kuwa nchi ya Urusi. Sehemu za magharibi ziliingizwa katika milki za Poland na Lithuania.

Leo hii nchi za Urusi, Ukraine na Belarus zinajitazama kama warithi wa Rus ya kihistoria.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.britannica.com/topic/Rus Rus, makala ya Encyclopedia Britannica online; wako pia wanahistoria Warusi wanaodai eti Warus walikuwa Waslavoni
  2. https://www.worldhistory.org/Kievan_Rus/ "Kievan Rus". World History Encyclopedia. Retrieved 24 May 2020.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • E. A. Melnikowa und Vladimir Jakovlevič Petrukhin: The origin and evolution of the name „Rus“. The Scandinavians in Eastern-European ethno-political processes before the 11th century. Thor 23 1991. [Tor: meddelanden från Institutionen för Nordisk Fornkunskap vid Uppsala Universitet / Institutionen för Arkeologi, Saerskilt Nordeuropeisk, Uppsala Universitet; Statens Humanistika Forskningsrad. – Uppsala
  • Håkon Stang: The Naming of Russia. Meddelelser, Nr. 77. University of Oslo Slavisk-baltisk Avelding, Oslo 1996.
Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rus kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.