Nenda kwa yaliyomo

Rupie ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rupie)
Rupie moja ya 1904
Rupia 1, upande wa nyuma; picha ya kaisari Wilhelm II (maandishi ya Kilatini: Guilelmus II Imperator)

Rupia ya Afrika Mashariki ya Ujerumani ilikuwa pesa rasmi ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kati ya 1890 na 1916 ikatumika katika Tanganyika hadi 1920.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa kuanzishwa kwa koloni ya Kijerumani, Rupia ya Uhindi ilikuwa pesa iliyotumiwa zaidi kwenye pwani ya Afrika ya Mashariki. Ilitumiwa zaidi kuliko Dolar ya Marekani na Dolar ya Maria Theresa. Mnamo mwaka 1890 Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki ilipata kibali cha serikali ya Kijerumani kutoa sarafu ikatoa "rupie" zilizolingana na rupia za Uhindi na Usultani wa Zanzibar. Kampuni hiyo ilibaki na haki ya kutengenezea sarafu hata baada ya serikali ya Ujerumani kuchukua mamlaka juu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Mnamo 1904 serikali ya Ujerumani ilichukua utoaji wa pesa mkononi mwake.

Hapo awali, rupie ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilikuwa sawa na ile ya Uhindi kwa thamani. Hadi mwaka 1904 ilikuwa imegawanywa kwa "pesa" 64 (sawa na paisa za Uhindi). Kuanzia Februari 1904, paisa zilifutwa na badala yake rupie iligawanywa kwa Heller 100. Wakati huo huo kiwango cha ubadilishaji ulifafanuliwa kuwa rupie 15 = Mark 20 za Ujerumani.

Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia benknoti za dharura zilitolewa.

Mnamo 1916 kulikuwa na toleo la mwisho la sarafu pamoja na sarafu ya dhahabu ya rupie 15, ambayo ilikuwa na thamani ya Mark 15 za dhahabu.

Mwaka uleule wa 1916, Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ilivamiwa na jeshi la Uingereza na Ubelgiji .

Katika maeneo ya Tanganyika, rupie ya Kijerumani iliendelea kutumiwa hadi 1920 pamoja na rupia ya Afrika ya Mashariki ya Kiingereza (ambayo ililingana kwa thamani) hadi 1920, wakati zote mbili zilifutwa na Florin ya Afrika Mashariki ilianzishwa kwa uwiano wa ubadilishaji wa 1: 1. Pale Burundi na Rwanda, Franc ya Kongo ya Kibelgiji ilichukua nafasi ya rupie mnamo 1916.

Mnamo mwaka 1890 sarafu ndogo za paisa 1 ya shaba na rupie 1 ya fedha zilianzishwa. Kwenye mwaka uliofuata sarafu za fedha za robo rupie na nusu rupie zilitolewa, mnamo 1893 pia sarafu za fesha za za rupie 2.

Baada ya kuhamia mfumo wa desimali mnamo 1904 sarafu za Heller zilitolewa kwa umbo la nusu heller, heller 1 na heller 5 za bronzi. Mwaka 1908 zilifuata heller 10 zilizokuwa sarafu zenye shimo katikati. 1913 walitoa pia heller 5 zenye shimo.

Wakati wa Vita Kuu sarafu za dhabu za rupie 15 pamoja na sarafu za dharura za heller 5 na heller 20 zilitolewa zilizotengenezwa katika karahana ya reli Tabora.

Benknoti

[hariri | hariri chanzo]

Mnamo mwaka wa 1905 Benki ya serikali ilitoa benknoti za rupie 5, 10, 50, 100 na 500. Kuanzia 1915 na tena 1917, benknoti za dharura zenye thamani ya rupie 1, 5, 10, 20, 50 na 200 zilitolewa.


Benknoti za dharura wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia
(matoleo ya 1915-17)
Thamani Mwaka Picha
1 Rupie 1915
Rupie 5 1915
Rupie 10 1916
Rupie 20 1915
Rupie 50 1915
Rupie 200 1915

Kujisomea

[hariri | hariri chanzo]
  • Krause, Chester L. na Clifford Mishler (1991). Katalogi Sanifu ya Sarafu za Ulimwenguni: 1801-1991 (ed. 18 Ed. ). Machapisho ya Krause. ISBN 0-87341-150-1 .
  • Chagua, Albert (1994). Katalogi ya Kawaida ya Pesa ya Karatasi Duniani: Maswala Ya Jumla. Colin R. Bruce II na Neil Shafer (wahariri) (7th ed. ). Machapisho ya Krause. ISBN 0-87341-207-9 .