Rose Mhando

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rose Muhando
Amezaliwa 1976
Kilosa, Morogoro
Nchi Tanzania
Kazi yake Msanii wa Muziki wa Injili
Dini Mkristo
Watoto tatu
Malkia wa nyimbo za Kiinjili.

Rose Mhando (pia akijulikana kama: Rose Muhando; amezaliwa Dumila, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, nchini Tanzania, 1976) ni msanii wa muziki wa Injili katika lugha ya Kiswahili maarufu kama malkia wa nyimbo za Kiinjili katika kanda ya Afrika Mashariki.

Rose, ambaye alikuwa muumini wa dini ya Kiislamu, ni mama wa watoto watatu. Mama huyu alidai kuwa akiwa na umri wa miaka tisa alipata maono ya Yesu Kristo akiwa amelazwa. Aliteseka kwa muda wa miaka mitatu, na baada ya hapo alipona na kubadili dini (kuongoka) na kuwa Mkristo.

Alianza fani yake ya muziki kama mwalimu wa kwaya inayoitwa Kwaya ya Mtakatifu Maria katika kanisa la kianglikana linaloitwa Chimuli mkoani Dodoma.

Mafanikio[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 31 Januari 2005, Rose Muhando alipata tuzo ya mtunzi bora, muimbaji bora, na tuzo ya msanii mwenye albamu bora ya mwaka wakati wa tamasha la tuzo za Kiinjili la mwaka 2004.

Mnamo Desemba 2005, alishiriki katika tamasha la Kiinjili ili kusaidia kutafuta fedha kwa ajili ya kituo cha watoto yatima cha Dar es salaam.

Baadhi ya albamu zake[hariri | hariri chanzo]

  1. Kitimutimu
  2. Uwe Macho 2004.
  3. Jipange Sawasawa 2008.[1][2].

Tuzo[hariri | hariri chanzo]

  • Mnamo mwaka 2005 Tuzo ya muziki, Tanzania: Mwimbaji bora wa kike na wimbo bora wa dini ( "Mteule uwe macho") [3]
  • 2009 Tuzo za Mwimbaji Bora wa Nyimbo za Injili Tanzania: Rose Mhando; Mwimbaji Bora Tanzania, alizawadiwa Tsh 200,000 na Shirika la Utangazaji la TBC chini ya mwavuli wa wimbo wake "Nibebe"
  • 2008 Kenya Tuzo za Groove - msanii bora wa kike wa injili barani Afrika

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Rose Mhando atia fora kwenye tamasha la Nane Nane", [1], 2004-08-14. Retrieved on 2007-05-12. Archived from the original on 2007-09-29. 
  2. "Mtanziko wa umaarufu wa Rose Mhando", [2], 2005. Retrieved on 2007-05-12. Archived from the original on 2006-06-15. 
  3. [4] ^Tuzo ya muziki, Tanzania: Washindi wa mwaka 2005
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rose Mhando kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.