Rosa Venerini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Rosa Venerini alivyochorwa.

Rosa Venerini (Viterbo, leo mkoani Lazio, Italia, 9 Februari 1656Roma, 7 Mei 1728) alikuwa bikira maarufu kwa huduma yake katika malezi ya wasichana. Kwa ajili hiyo alianzisha shule ya kwanza kwa wasichana tu nchini Italia, halafu shirika la masista walimu linalodumu hadi leo. Alipofariki shule zake zilikuwa 40 tayari.

Papa Pius XII alimtangaza mwenye heri tarehe 4 Mei 1952, halafu Papa Benedikto XVI akamtangaza mtakatifu tarehe 15 Oktoba 2006[1].

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyoaga dunia[2][3].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Vatican News Service
  2. Martyrologium Romanum
  3. "St. Rosa Venerini", Catholic News Agency
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.