Robert Huth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Robert Huth akichezea Middlesbrough mwaka 2009

Robert Huth (alizaliwa Biesdorf, mashariki mwa Berlin, Ujerumani, tarehe 18 Agosti 1984) ni mchezaji wa mpira.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Utotoni alichezea soka katika timu ya mtaani Vfb Forfuna Biesdorf, kisha Feunion Berlin.

Alichezea timu za Chelsea, pia Bayern Munich walimtaka lakini hawakufanikiwa, akaenda Middlesbrough.

Baada ya miaka miwili akaenda Stoke City aliichezea mechi ya 100 katika ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Evarton mnamo 4 Oktoba 2009.

Msimu wa 2010/2011 aliisaidia Stoke City kucheza fainali za FA na kufungwa na Manchester City goli 1-0 na Huth alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Stoke City.

Mwaka 2013 aliumia na kufanyiwa operesheni ambazo zilimweka nje msimu mzima na mwanzoni mwa 2014/2015 akaumia tena na kukaa nje kwa miezi miwili ambapo alirudi 9 Desemba 2014 akacheza dhidi ya Arsenal.

Kwa misimu 6 alikuwa amechezea mechi 188.

Tarehe 2 Februari 2015 hult alitua Leicester City kwa mkopo mpaka mwishoni mwa msimu: kuwasili kwa Huth kulisababisha washinde mechi 9 za mwisho na kubaki ligi kuu.

Baada ya kusajiliwa na Leicester tarehe 24 Juni 2015, Huth amekuwa tegemeo kubwa kwenye kikosi hadi kukiwezesha kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza mwaka 2016.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Robert Huth kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.