Nenda kwa yaliyomo

Darubini ya redio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Radio telescope)
Darubini ya redio ya mita 64 katika Parkes Observatory kama ilivyoonekana mwaka wa 1969, wakati ilitumiwa kupokea video ya moja kwa moja kutoka Apollo 11.
Antena ya darubini ya redio ya masafa ya dekamita, mkoa wa Kharkiv, Ukraine .
"Very Large Array" katika New Mexico ni mpangilio wa dishi 27 zinazokusanya vipimo kwa pamoja.
Darubiniredio ya FAST nchini China ina kipenyo cha mita 500

Darubini ya redio ni antena maalum na kipokeaji cha redio kinachotumiwa kutambua mawimbi ya redio kutoka kwa vyanzo vya redio kwenye anga-nje. [1] [2] [3] Darubini za redio ndizo vyombo vikuu vya uchunguzi vinavyotumika katika astronomia redio, ambayo huchunguza mawimbi ya redio yanayotolewa na violwa vya anga-nje kama vile nyota, galaksi au nebula. Hivyo zinalingana na darubini nuru zinazochungulia mawimbi ya nuru yanaotoka kwenye violwa vya anga-nje. Tofauti na darubini za nuru, darubini za redio zinaweza kutumika wakati wa mchana na usiku[4].

Vyanzo vya ishara

[hariri | hariri chanzo]

Vyanzo vya redio vya kiastronomia kama vile nyota, nebula na galaksi viko mbali sana, mawimbi ya redio yanayotoka humo ni dhaifu sana. Kwa hiyo darubini za redio zinahitaji antena kubwa sana kukusanya nishati ya redio ya kutosha ili kuzichunguza, pamoja na vifaa nyeti sana vya kupokea.

Darubini za redio mara nyingi ni antena kubwa za dishi ("sahani") zinazofanana na zile zinazotumika kupokea mawimbi kutoka satelaiti kwa ajili ya runinga.

Dishi hizo zinaweza kutumika moja moja au kwa nyingi zikiunganishwa pamoja kielektroniki.

Paoneaanga za redio hupangwa kuwa mbali na miji mikubwa au maneo penye watu wengi ili kuepuka kuingiliwa na ishara za sumakuumeme (EMI) kutoka kwa redio, televisheni, rada, magari, simu na vifaa vingine vya kielektroniki.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mawimbi ya redio kutoka angani yaligunduliwa kwa mara ya kwanza na mhandisi Karl Guthe Jansky mwaka wa 1932 katika huko Marekani kwa kutumia antena iliyojengwa kuchunguza mapokezi ya redio.

Darubini ya redio ya kwanza iliyojengwa kimakusudi ilikuwa dishi yenye kipenyo cha mita 9 iliyojengwa na mwanaridhaa ya redio Grote Reber karibu na nyumba yake huko Wheaton, Illinois mnamo 1937. Uchunguzi wa anga aliofanya huchukuliwa mara nyingi kuwa mwanzo wa astronomia ya redio[5].

Antena kubwa

[hariri | hariri chanzo]

Kifaa kikubwa duniani ni darubiniredio ya RATAN-600 karibu na Nizhny Arkhyz nchini Urusi inayofanywa na duara ya viakisi yenye kipenyo cha mita 576.

Dishi kubwa duniani iliyojaa ni darubiniredio ya FAST (Five-hundred-meter Aperture Spherical Telescope) iliyokamilika mwaka 2016 nchini China [6]. Ina kipenyo cha mita 500. Inafanywa na viakisi 4,450 na kila moja kinaweza kusogezwa na kulengwa hadi nyui 40° juu ya upeo wa macho.

Dishi kamili kubwa ya pili ilikuwa darubiniredio ya Arecibo huko Puerto Rico yenye kipenyo cha mita 305 iliyoporomoka kwenye disemba 2020. Haikuwa kipokeaji pekee lakini iliweza pia kurusha miale ya rada.

Darubiniredio hizo kubwa zinalengwa kiasi tu; haziwezi kugeuzwa kwa jumla.

Darubiniredio kubwa zaidi duniani zinazoweza kugeuzwa na kulengwa pote ni Green Bank Telescope yenye kipenyo huko West Virginia, Marekani na darubiniredio ya Effelsberg, Ujerumani zenye kipenyo cha mita 100[7].

Mipangilio ya darubiniredio

[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 1946 kuna tekinolojia ya kuunganisha antena tofauti zinazoiga antena moja kubwa. Antena hizo huunganishwa katika mpangilio (array) zikitumia maingiliano ya mawimbi (wave interference) na mbinu huu unaruhusu kupata ufumbuzi mzuri zaidi yaani ukuzaji[8].

Tekinolojia hiyo imeendelea hivyo inawezekana pia kurekodi ishara ya kila antena peke yake na kuziunganisha baadaye. Hii inaruhusu kutumia antena zilizo mbali kati yao. Mfano wa mbinu huu ni Mpangilio wa Kilomita ya Mraba (Square Kilometre Array - SKA) inayojengwa huko Australia na Afrika Kusini ilhali ishara za vituo vyake vitaunganishwa kwenye paoneanga pa Jodrell Bank huko Uingereza.[9]

Recent advances in the stability of electronic oscillators also now permit interferometry to be carried out by independent recording of the signals at the various antennas, and then later correlating the recordings at some central processing facility.

  1. Marr, Jonathan M.; Snell, Ronald L.; Kurtz, Stanley E. (2015). Fundamentals of Radio Astronomy: Observational Methods. CRC Press. ku. 21–24. ISBN 978-1498770194.
  2. Britannica Concise Encyclopedia. Encyclopædia Britannica, Inc. 2008. uk. 1583. ISBN 978-1593394929.
  3. Verschuur, Gerrit (2007). The Invisible Universe: The Story of Radio Astronomy (tol. la 2). Springer Science & Business Media. ku. 8–10. ISBN 978-0387683607.
  4. What are radio telescopes? tovuti ya National Radio Astronomy Observatory, Marekani, iliangaliwa Machi 2023
  5. Sullivan, W.T. (1984). The Early Years of Radio Astronomy. Cambridge University Press. ISBN 0-521-25485-X
  6. "China Exclusive: China starts building world's largest radio telescope". English.peopledaily.com.cn. 2008-12-26. Iliwekwa mnamo 2016-02-24.
  7. https://www.mpifr-bonn.mpg.de/en/effelsberg Radio Telescope Effelsberg, tovuti ya Taasisi ya Max Planck, iliangaliwa Machi 2023
  8. https://www.ita.uni-heidelberg.de/~dullemond/lectures/obsastro_2011/chap_interferometry.pdf Interferometry: The basic principles (PDF); tovuti ya Institute of Theoretical Astrophysics, Chuo Kikuu cha Heidelberg, iliangaliwa Machi 2023
  9. https://www.skao.int/en/about-us/skao One global observatory operating two telescopes on three sites, tovuti ya SKAO, iliangaliwa Machi 2023

Kusoma zaidi

[hariri | hariri chanzo]
    • Rohlfs, K., & Wilson, T. L. (2004). Tools of radio astronomy. Astronomy and astrophysics library. Berlin: Springer.
    • Asimov, I. (1979). Isaac Asimov's Book of facts; Sky Watchers. New York: Grosset & Dunlap. pp. 390–399. ISBN 0-8038-9347-7ISBN 0-8038-9347-7