QR code

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mfano wa QR code

QR code (au Msimbo wa QR; kutokana na Kiingereza Quick Response Code) ni maandishi au picha zilizo na mpangilio maalumu ambazo huweza kusomeka kwa kutumia kifaa maalum kama simu janja (smartphone) ambayo huweza kutumia kamera kusoma hayo maandishi au picha ili kuweza kutambua data zilizoko ndani msimbo pau (barcode).

Teknolojia hii iliundwa huko Japani kwa ajili ya sekta ya magari ingawa hivi sasa inatumika katika sekta nyingine pia. Teknolojia hii ilipata maarufu nje ya sekta ya magari kutokana na usomaji wake wa haraka na uwezo mkubwa wa kuhifadhi data ikilinganishwa na msimbo pau wa UPC. Mambo ambayo teknolojia hii inaweza kuyashughulikia ni pamoja na kufuatilia bidhaa, wakati, nyaraka, kitambulisho cha bidhaa n.k.

Msimbo huu huwa na miraba miyeusi iliyopangwa kwa mraba fito na rangi nyeupe nyuma yake ambayo inaweza kusomwa na kifaa kama kamera.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]