Pyrrhus
Pyrrhus au Pyrrhos (kwa Kigiriki: Πύρρος της Ηπείρου, Pyrrhos tes Epeiru; 319–272 KK) alikuwa mfalme wa Epirus katika Ugiriki ya Kale wa enzi ya Uheleni.
Alizaliwa baada ya kifo cha Aleksander Mkuu, kwa hiyo alikuwa mtoto wakati wa mvurugo wa mapambano baina ya majenerali wa Aleksander Mkuu. Kwa msaada wa Ptolemaio I wa Misri aliweza kushika urithi wa baba yake na kuwa mfalme[1].
Mnamo mwaka 280 KK aliitikia ombi la mji wa Kigiriki Taranto kusini mwa Italia uliotafuta msaada dhidi ya upanuzi wa Jamhuri ya Roma.[2]
Kwa msaada wa wafalme wengine wa Ugiriki alikusanya jeshi la askari wa miguu 20.000, askari farasi 3.000, wapiga mishale 2.000, wapiga manati 500 na tembo wa vita 20. Baada ya kufika Italia alishinda jeshi la Roma katika mapigano mawili. Hata hivyo, alipoteza askari wengi hadi kusema "ushindi mmoja tena wa namna hii na tutakuwa tumekwisha"[3]. Kwa hiyo ushindi unaoleta hasara kubwa kwa mshindi huitwa "ushindi wa Pyrrhus" (kwa Kiing. Pyrhic victory).
Baada ya mapigano mengine alishindwa na Waroma huko Benevento kwenye mwaka 275 KK na hapo alirudi Ugiriki. Alikuta nchi katika hali ya vita kati ya milki ndogo. Wakati wa kuvamia mji Argos aliuawa katika mapigano.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Champion 2009, p. 18.
- ↑ https://www.britannica.com/biography/Pyrrhus
- ↑ Plutarch, Maisha ya Pyrrhus, tovuti ya Chuo kikuu cha Chicago
Kujisomea
[hariri | hariri chanzo]- Abbott, Jacob (1901). Makers of History: Pyrrhus. New York and London: Harper & Brothers Publishers.
- Cowan, Ross (2009). Roman Conquests: Italy. Barnsley: Pen & Sword Books Limited. ku. 103–147. ISBN 978-1-84-415937-6.
- Cowan, Ross (2007). For the Glory of Rome: A History of Warriors and Warfare. London: Greenhill Books. ku. 15–77. ISBN 978-1-85-367733-5.
- Franke, P. R. (1989). "CHAPTER 10 PYRRHUS". Katika Astin, A. E.; Walbank, F. W.; Frederiksen, M. W.; Ogilvie, R. M.; Drummond, A. (whr.). The Cambridge Ancient History: The Rise of Rome to 220 BC. Juz. la VII, Part 2. Cambridge: Cambridge University Press. ku. 456–485. ISBN 0-521-23446-8.
- Leveque, Pierre (1957). Pyrrhos. Paris: E. de Boccard.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Pyrrhus of Epirus on Livius.org
- "Pyrrhus". Encyclopædia Britannica (11th ed.). 1911.