Nenda kwa yaliyomo

Kipolandi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Pol.)
Kipolandi
Polski (pl)
Lugha
Asili Polandi
Wasemaji

L1 : Takriban 40 Milioni
L2: Takriban 2.1 Milioni

Jumla: 42 Milioni
Familia za lugha Kihindi-Kiulaya
Kislaviki
Kislaviki cha Magharibi
Kilehita
Aina za Awali Kislaviki cha Kale
Mfumo wa kuandika Alfabeti ya Kilatini (toleo la Kipolandi)
Lugha Rasmi
Lugha rasmi kwa Polandi
Nambari za Msimbo
ISO 639-1 pl
ISO 639-2 pol
Glottolog poli1260

Kipolandi (kwa lugha asilia: polski) ni lugha ya Kislavoni cha Magharibi inayozungumzwa hasa nchini Polandi. Ni lugha rasmi ya taifa hilo na inazungumzwa na takribani watu milioni 40 kama lugha ya kwanza, pamoja na zaidi ya milioni 2.1 wanaoitumia kama lugha ya pili, hususan miongoni mwa jamii za Kihamiaji barani Ulaya, Amerika Kaskazini, na Australia. Kipolandi ni mojawapo ya lugha kubwa zaidi katika familia ya lugha za Kislaviki, na hutumia alfabeti ya Kilatini yenye herufi 32, zenye alama za matamshi za kipekee kama vile ą, ć, ę, ł, ń, ó, ś, ź, ż.

Kipolandi kina historia ndefu na tajiri, kimeathiriwa na lugha nyingine za Ulaya kama vile Kijerumani, Kilatin, na Kirusi, hasa katika nyanja za fasihi, siasa na elimu. Fasihi ya Kipolandi imechangia kwa kiasi kikubwa utamaduni wa Ulaya Mashariki, na waandishi wa Kipolandi kama Adam Mickiewicz na Wisława Szymborska wametambuliwa kimataifa. Leo hii, Kipolandi pia hutumika katika taasisi za Ulaya kama mojawapo ya lugha rasmi za Umoja wa Ulaya, na ni lugha muhimu katika biashara, elimu ya juu, na diplomasia katika kanda ya Ulaya ya Kati.

Kuna takriban herufi 9 za Kipolandi ambazo katika Kiingereza hakuna. Zinaonekana kuwa kama Kiingereza, lakini zenyewe zinaviji alama kwa juu au kwa chini.

Katika herufi ndogo, herufi tisa ni: ą ć ę ł ń ó ś ź ż

Katika herufi kubwa, herufi tisa ni: Ą Ć Ę Ł Ń Ó Ś Ź Ż

Kuna herufi 3 katika Kiingereza ambazo katika Kipolandi hazitumiki: q, v, x.

Kuna mchanganyiko wa herufi 7 katika kila herufi 2 ambazo zote zinaonekana kuwa kama sawa katika kusikika (ambazo sawa na "th" au "qu" katika Kiingereza). Ambazo zimejumlisha herufi kama vile "ch", "cz", "dz", "dź", "dż", "rz", "sz", "szcz".

Kusikika

[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Kipolandi ina lafudhi nyingi sana, lakini ni chache mno kuliko lugha zingine za Ulaya. Kuna utofauti mdogo tu katika Kipolandi cha "kawaida", lakini kila mwongeaji anaweza kumwelewa mwenziwake, na wale ambao wao sio wazawa wa lugha hiii kawaida hawezi kujua tofauti zao katika kutamka.

Maneno kadhaa ya Kipolandi

[hariri | hariri chanzo]

ja - mimi
ty - wewe
on - yeye
my - sisi
oni - wao

co? - nini?
kto? - nani?
gdzie? - mahali gani?
dokąd? - wapi?
kiedy? - hini?
jak? - vipi?
dlaczego? - kwanini?
który? - ipi?

Namba:

moja - jeden
mbili - dwa
tatu - trzy
nne - cztery
tano - pięć
sita - sześć
saba - siedem
nane - osiem
tisa - dziewięć
kumi - dziesięć
kumi na moja - jedenaście
kumi na mbili - dwanaście
ishirini - dwadzieścia
ishirini na moja - dwadzieścia jeden
thelathini - trzydzieści
arobaini - czterdzieści
hamsini - pięćdziesiąt
mia moja - sto
elfu moja - tysiąc

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]