Cheruku
Mandhari
(Elekezwa kutoka Pluvianus)
Cheruku | ||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||
| ||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||
Jenasi 3:
|
Cheruku ni ndege wa jenasi mbalimbali katika familia Glareolidae. Ndege hawa wanaweza kukimbia sana. Wanatokea mahali pakavu kama nyika au jangwa. Hula nzige na wadudu wengine na huyataga mayai mchangani. Cheruku-mamba huonekana karibu na mito na hutaga mayai yake kwa mafungu ya mchanga mtoni. Huainishwa na wataalamu wengine katika familia Pluvianidae. Spishi hii hula wadudu lakini pia hutoa nyama kwa kati ya meno ya mamba.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Cursorius cursor, Cheruku Kaskazi (Cream-coloured Courser)
- Cursorius rufus, Cheruku wa Burchell (Burchell's Courser)
- Cursorius somalensis, Cheruku Somali (Somali Courser)
- Cursorius temminckii, Cheruku Utosi-mwekundu (Temminck's Courser)
- Pluvianus aegyptius, Cheruku-mamba (Egyptian Plover au Crocodile Bird)
- Rhinoptilus africanus, Cheruku Mikufu-miwili (Double-banded Courser)
- Rhinoptilus chalcopterus, Cheruku Mabawa-shaba (Bronze-winged Courser)
- Rhinoptilus cinctus, Cheruku Mikufu-mitatu (Three-banded Courser)
Spishi za Asia
[hariri | hariri chanzo]- Cursorius coromandelicus (Indian Courser)
- Rhinoptilus bitorquatus (Jerdon's Courser)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Cheruku wa Burchell
-
Cheruku utosi-mwekundu
-
Cheruku-mamba
-
Cheruku mikufu-miwili
-
Cheruku mikufu-mitatu
-
Indian courser