Pinokyo (mhusika)
Pinokyo (kwa Kiitalia jina linalotamkwa hivyo linaandikwa Pinocchio) ni mhusika katika vitabu vya Mambo yalioyompata Pinokyo vilivyoandikwa na Carlo Collodi.
Simulizi la Pinokyo
[hariri | hariri chanzo]Siku moja seremala Maestro Ciliegia anakuta kipande cha ubao kinachoanza kusema akitaka kukikata. Kwa kuogopa anampa rafiki yake Geppetto (jina linasomeka Jepeto) aliye mchongaji. Geppetto anatumia ubao huo kuchonga karagosi anayeendelea kusema na mara baada ya kukamilika anatoroka. Akirudi nyumbani kwa njaa anaahidi kuwa mtoto mzuri na mtiifu lakini baada ya muda anatoroka tena. Anapatwa na shani nyingi hadi kukutana na baba yake Geppetto ndani ya tumbo la nyangumi. Pamoja wanajiokoa na Pinokyo anaahidi tena kuwa mtoto mzuri na safari hii anaacha utundu wake. Baada ya kutenda mema, anaamka siku moja anajikuta amebadilika umbo lake na sasa yu mvulana mwenye mwili wa kibinadamu.
Pua la Pinokyo lina tabia ya pekee; kila anaposema uwongo pua lake linakua kuwa ndefu zaidi. Kwa hiyo hawezi kuficha uwongo, na tbia hiyo ya pua inamsaidia kuachana na uwongo.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya fasihi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Pinokyo (mhusika) kama historia yake, uenezi au maendeleo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |