Paulo Ge Tingzhu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Paulo Ke Tingzhou)
Wafiadini Wakatoliki wa China.

Paulo Ge Tingzhu (Xiaotun, 1839 hivi - Xiaotun, 8 Agosti 1900) alikuwa mlei wa China aliyefia Ukristo wakati wa Uasi wa Waboksa.

Kiongozi wa Wakristo wa kwao alinyofolewa nyama kipande baada ya kipande, akiwapa wenzake kielelezo kizuri ajabu cha nguvu kwa kuvumilia yote bila kuyumba[1].

Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wengine 119 tarehe 1 Oktoba 2000.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 9 Julai, ila ya kwake mwenyewe katika tarehe ya kifodini chake[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.