Paul George

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
George akiwa na timu ya Indiana Pacers 2014

Paul Clifton Anthony George (amezaliwa Mei 2, 1990) ni mchezaji wa mpira wa kikapu wa kimarekani anaechezea timu ya Los Angeles Clippers[1] katika chama cha mpira wa kikapu Marekani (NBA). Aitwaye "PG-13", yeye ni nyota wa muda wote wa NBA mara nane na mwanachama mara sita wa Timu ya All-NBA, na pia mwanachama mara nne wa timu ya ulinzi ya NBA All-Defensive.

George alicheza mpira wa kikapu wa shule za sekondari akiwa na timu ya shule ya sekondari Knight kabla ya kucheza misimu miwili ya mpira wa kikapu wa vyuo vikuu akiwa na timu ya chuo kikuu cha Fresno State Bulldogs.[2] Alichaguliwa na timu ya Indiana Pacers chaguo la 10 la jumla ya drafti ya NBA ya 2010, na akapata tuzo ya timu ya pili ya heshima NBA All-Rookie. Alitajwa kama mchezaji aliyeboreshwa zaidi wa NBA mnamo 2013, pia alipata uteuzi wake wa kwanza wa kuwa nyota (All-Star).

George alivunjika mguu mwaka wa 2014 alipokuwa akiwania nafasi ya kuorodheshwa kwenye timu ya taifa ya mpira wa kikapu ya Marekani kwa ajili ya kombe la Dunia la mpira wa kikapu la FIBA. Alikosa sehemu kubwa ya msimu wa 2014-2015, lakini akapata nafuu na kuwa nyota (All-star) tena mnamo 2016, wakati pia alishinda medali ya dhahabu ya Michezo ya Olimpiki. Aliuzwa kwenda kwenda kuchezea timu ya Oklahoma City Thunder mnamo 2017, na alicheza misimu miwili akiwa Thunder kabla ya kuuzwa tena na kwenda kuchezea timu ya Clippers mnamo 2019.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Bruno Manrique (2017-07-15). "The Truth About Paul George's Basketball Allegiance To The City Of Los Angeles". ClutchPoints (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-05-19. 
  2. "Better Know a Prospect: Paul George, G - Fresno State - At The Hive". web.archive.org. 2010-12-24. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-12-24. Iliwekwa mnamo 2023-05-19.