FIBA AfroBasket 2017

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

FIBA AfroBasket 2017 yalikuwa ni mashindano ya 29 kuandaliwa na AfroBasket, ubingwa wa bara la Afrika wa mpira wa kikapu kwa wanaume.[1] Mashindano hayo yaliandaliwa na nchi mbili Tunisia na Senegal.[2] Angola iliomba FIBA Africa kuandaa mashindano hayo, maombi yao yalikataliwa kwani nchi hiyo ilikuwa na uchaguzi mkuu mwaka huo.[3]

Tunisia ilishinda taji lao la pili baada ya kuishinda Nigeria 77-65 katika mchezo wa fainali, huku Senegal ikikamata nafasi ya tatu kwa kuishinda Moroko 73-62.[4]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "FIBA AfroBasket 2017", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2021-11-03, iliwekwa mnamo 2022-09-04 
  2. "FIBA AfroBasket 2017", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2021-11-03, iliwekwa mnamo 2022-09-04 
  3. "FIBA AfroBasket 2017", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2021-11-03, iliwekwa mnamo 2022-09-04 
  4. "Tunisia crowned FIBA AfroBasket 2017 Champions". FIBA.basketball (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-09-04.