Paul Ereng
Paul Ereng (alizaliwa 22 Agosti 1966) ni mwanamichezo wa zamani wa Kenya na mshindi wa mbio ya 800m katika Olimpiki ya 1988 huku akiwashangaza watu.
Maisha ya hapo awali
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa Kitale(katika Wilaya ya Trans-Nzoia) nchini Kenya, Paul Ereng alisomea Shule ya Upili ya Starehe mjini Nairobi. Yeye alikuwa anaonekana kama alikuwa bora katika mbio ya 400m hadi mwisho wa mwaka wa 1988. Baada ya kujiandikisha katika Chuo Kikuu cha Virginia, Ereng alianza kukimbia mbio ya 800m,hapo mwanzo wa 1988.
Maisha katika Riadha
[hariri | hariri chanzo]Ereng hakuwahi shindwa katika msimu wa Marekani wa mbio za nje katika mwanzo wa mwaka wa 1988. Yeye alishinda taji la NCAA 800 m katika miaka ya 1988 na 1989. Lakini katika majaribio ya timu ya Olimpiki ya Kenya,Ereng alihitimu kwa kidogo tu kwa kumaliza katika nafasi ya tatu. Ingawa alikuwa anakua kwa kasi sana,Ereng hakuonekana kama mshindi wa dhahabu alipowasili Seoul kwa michezo hiyo ya Olimpiki. Hata hivyo, watu walianza kumsifu na kuona umaarufu wake aliposhinda semi fainali yake na muda wa 1:44.55,uliokuwa muda wake bora wa wakati huo.
Katika fainali ya Olimpiki, Ereng alikuwa katika nafasi ya nne ,walipoingia mkondo wa mwisho, lakini alitimua mbio na akawapita wanariadha wote watatu ili kushinda medali ya dhahabu. Baada ya Olimpiki, alirudi nyumbani Kenya na kukaribishwa kama shujaa. Jambo bora zaidi lilikuwa kupokea medali yake(tena) katika mkutano wa jioni wa shule ya Starehe kutoka kwa marehemu Dkt. Geoffrey William Griffin.Katika Mbio ya Ndani ya Ukumbi ya Dunia mjini Budapest,Ereng alikimbia kasi tena katika mkondo wa mwisho na kushinda medali ya dhahabu katika rekodi mpya ya mbio za ndani ya ukumbi katika muda wa 1:44.84.
Katika mwaka wa 1991, Ereng alishinda tena taji lake la mbio ya ndani ya ukumbi akiwa Seville lakini akawa # 4 katika Mbio ya Dunia ya Ubingwa mjini Tokyo. Ereng hakuwa tisho tena katika mbio za kimataifa baada ya hiyo na akashindwa katika semi fainali ya Olimpiki ya 1992.
Masomo na kazi
[hariri | hariri chanzo]Ereng alifuzu kutoka Virginia katika mwaka wa 1993 akiwa na shahada ya digrii ya ukapera katika masomo ya kidini na shahada ndogo ya elimu ya jamii(sociolojia). Yeye anamiliki shamba la ekari 50 Kitale. Mkewe, Fatima,alikuwa mkuu wa mauzo katika Kundi la Nation Media.
Hivi sasa,yeye anafanya kazi kama kocha wa Riadha katika Chuo Kikuu cha Texas, El Paso.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Daily Nation, 3 Juni 2000: Bingwa bado yu hai na anafanya mambo
- Daily Nation, 3 Juni 2000:Baada ya kushinda dhahabu
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Paul Ereng katika IAAF Archived 20 Oktoba 2012 at the Wayback Machine.
- Kuhusu Paul Ereng Archived 8 Julai 2011 at the Wayback Machine.
- Mahojiano ya Video ya Paul Ereng katika tovuti ya Flotrack.com