Paco Alcácer

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alcácer akijiandaa kabla ya mechi.

Francisco Paco Alcácer García (anajulikana sana kama Alcácer; alizaliwa 30 Agosti 1993) ni mchezaji wa soka wa Hispania ambaye anacheza kama mshambuliaji wa klabu ya Ujerumani Borussia Dortmund na timu ya taifa ya Hispania.

Alianza kazi yake na vijana wa klabu ya Valencia, Alianza kucheza na timu ya kwanza mnamo 2010, Alikuwa mchezaji wa mkopo huko Getafe, Alifunga jumla ya mabao 57 katika mechi 118. Mnamo mwaka 2016, alisaini mkataba kwenda Barcelona kwa milioni 30, alishinda makombe mawili ya Copa del Rey na moja la La Liga.

Mnamo 28 Agosti 2018, Alcácer alijiunga na timu ya Bundesliga Borussia Dortmund kwa mkopo wa muda mrefu. Na Dortmund walipewa chaguo la kumnunua au kutomnunua.

Alcacer alionesha kiwango cha juu sana na kufunga mabao mengi kuliko wachezaji wote kwenye timu, Klabu ilitumia chaguo lao la kumnunua moja kwa moja kwa € milioni 23 mpaka 2024.

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paco Alcácer kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.