Pérrine Moncrieff CBE

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Pérrine Moncrieff CBE (8 Februari 1893 - 16 Disemba 1979) alikuwa mwandishi, mhifadhi na mtaalamu na mtafiti wa aina za ndegepori nchini New Zealand.[1]

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa London, Uingereza mwaka 1893 alijulikana kama Pérrine Millais.[1] Alikuwa binti mkuu wa mchoraji Sir John Millais. Alitumia maisha yake ya utotoni akiishi London, Brussels na Perthshire huko Scotland. Aliolewa na Kapteni Malcolm Moncrieff, mnamo mwaka 1914. Walihama Uingereza hadi New Zealand baada ya Vita vya Kwanza vya dunia. [2] Alikuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Muungano wa Royal Australasian Ornithologists Union (RAOU), 1932-1933. Alijiunga na shirika kwa mara ya kwanza mnamo 1923 na miaka miwili baadaye alichapisha kitabu cha "New Zealand birds and how to identify them". Kitabu hicho kilifanikiwa, na matoleo sita yalichapishwa kuanzia mwaka 1925 hadi 1961.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Kigezo:DNZB
  2. Secker, HL (1980). "Obituary. Perrine Millais Moncrieff". Emu 80 (3): 171. doi:10.1071/mu9800171. 
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pérrine Moncrieff CBE kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.