Nenda kwa yaliyomo

Oberkappel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jagdschloss Schöffgattern.
Mchoro wa ukutani kanisani.

Oberkappel ni manispaa nchini Austria kwenye jimbo la Austria ya Juu, iliyoko katika wilaya Rohrbach (RO). Manispaa ina wakazi wapatao 800.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Oberkappel ina eneo la km² 12. Manispaa iko katika jimbo la Austria ya Juu, kwenye ncha ya kaskazini ya Austria. Mipaka ya Ujerumani na Jamhuri ya Cheki iko karibu.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kwenye karne za kati, Oberkappel ilikuwa sehemu ya utawala wa maaskofu wa Passau. Ilikuwa sehemu ya parokia Wegscheid hadi kuwa parokia ya pekee mnamo mwaka 1783. Wakati wa kumalizika kwa utawala wa kiaskofu mnamo 1803 ilipelekwa upande wa utemi wa Salzburg, ikahamishwa kwa miaka michache upandew wa Bavaria na tangu 1814 imekuwa tena upande wa Austria ya Juu.

Wakati wa Vita vya Pili vya Dunia Oberkappel ndipo ambapo wanajeshi wa mataifa ya ushirikiano waliingia kwa mara ya kwanza katika eneo la Austria. Leo Oberkappel ni mji mdogo wa watalii.

Michezo na burudani[hariri | hariri chanzo]

Kuna njia za matembezi kwa miguu za Kiulaya E8 na E10 ambazo zinapita hapa. E8 inaanzia Ireland kupitia, miongoni mwa nchi nyingine, Uholanzi (inayoitwa Oeverloperpad na Lingepad nchini Uholanzi), Ujerumani, Austria kaskazini na Slovakia hadi mipaka ya Poland na Ukraine. E10 inatoka Lapland na inasafiri kupitia Ufini, Ujerumani, Ucheki na Austria hadi Bozen/Bolzano kaskazini mwa Italia; Kuna mipango ya kuendeleza njia kupitia Ufaransa na pwani ya mashariki ya Hispania hadi Gibraltar.

Wakazi maarufu[hariri | hariri chanzo]