Nenda kwa yaliyomo

Wakarmeli Peku

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka O.C.D.)
Nembo ya shirika.

Wakarmeli Peku (kwa Kilatini Ordo Fratrum Discalceatorum B. Mariae V. de Monte Carmelo, kifupi O.C.D.) ni watawa wa Kanisa Katoliki wanaofuata urekebisho wa shirika la Wakarmeli ulioanzishwa na Teresa wa Yesu katika karne ya 16 huko Hispania. Upande wa wanaume alisaidiwa na Yohane wa Msalaba.

Mbali ya waanzilishi hao wawili, shirika lilizaa mwalimu wa Kanisa mwingine, Teresa wa Mtoto Yesu katika karne ya 19.

Kwa jumla hao watatu wanatazamwa kuwa viongozi bora kuhusu kuzama katika sala na maisha ya kiroho kwa jumla.

Pia shirika lilizaa watakatifu na wenye heri wengi.

Mwishoni mwa mwaka 2005 shirika lilikuwa na nyumba 572 zenye watawa 4067, (kati yao mapadri 2655).[1]

  1. Annuario Pontificio per l'anno 2007, Città del Vaticano, 2007, p. 1467

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]