Nenda kwa yaliyomo

Makumbusho ya Kitaifa Dar es Salaam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nyumba ya Makumbusho)
Makumbusho ya Kitaifa Dar es Salaam, jengo la King George V.

Makumbusho ya Kitaifa Dar es Salaam ni jengo la makumbusho lililoko jijini Dar es Salaam, kwenye sehemu ya kihistoria ya Ilala mkabala wa barabara ya Shaban Robert na Samora nchini Tanzania.

Chanzo cha makumbusho ni jengo dogo lililofunguliwa mwaka 1940 kwa heshima ya Mfalme George V wa Uingereza aliyetawala Tanganyika wakati ule. Jengo hilo lilijengwa kwa mtindo wa ubunifu wa Kiarabu.

Makumbusho hayo yamepanuliwa kwa majengo ya kisasa yenye sehemu ya sayansi, ya elimu na ya utamaduni ambayo yanahusika na kukusanya, kuhifadhi, kusambaza na kuvumbua mambo ya kihistoria na utamaduni.

Nyumba hiyo ya makumbusho inahifadhi mali na vitu mbalimbali vilivyovumbuliwa na kugunduliwa ambavyo vinahifadhiwa kwa ajili ya kumbukumbu kwa kizazi cha sasa na cha baadaye ili kuweza kujua tulitoka wapi.

Katika nyumba hiyo ya makumbusho kuna vitu mbalimbali vilivyohifadhiwa ikiwemo michoro ya mapangoni, nyayo za zamadamu, historia ya mabadiliko ya mwanadamu, sanaa na mambo mengine mengi ya kihistoria.

Makumbusho hayo ya Dar es Salaam ni sehemu ya Makumbusho ya Kitaifa ya Tanzania, pamoja na Kijiji cha Makumbusho Dar es Salaam, Makumbusho ya Historia Asilia na Makumbusho ya Azimio la Arusha mjini Arusha, na Makumbusho ya Nyerere huko Butiama alikozaliwa.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Makumbusho ya Kitaifa Dar es Salaam kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.