Nenda kwa yaliyomo

Nyoka mdomo-kulabu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyoka mdomo-kulabu
Nyoka mdomo-kulabu (Scaphiophis albopunctatus)
Nyoka mdomo-kulabu (Scaphiophis albopunctatus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Colubridae (Nyoka walio na mnasaba na kipiri)
Oppel, 1811
Nusufamilia: Colubrinae (Nyoka wanaofanana na kipiri)
Oppel, 1811
Jenasi: Scaphiophis
[[[Wilhelm Peters|W. Peters]], 1870
Ngazi za chini

Spishi 2:

Nyoka mdomo-kulabu ni nyoka wa jenasi Scaphiophis katika familia Colubridae. Wamepewa jina hili kwa sababu mdomo wa juu una umbo wa kulabu kama domo la kipanga.

Nyoka hawa ni warefu kiasi, m 1.6 kwa kipeo lakini m 0.9-1.3 kwa kawaida. Rangi ya mgongo ni kijivu au kahawia, ile ya mbavu ni kijivu, kahawia, kahawianyekundu au machungwa na ile ya tumbo machungwa, pinki au maziwa. Ndani ya mdomo ni nyeusi.

Nyoka mdomo-kulabu huishi katika vishimo au huchimba katika udongo tifutifu. Hula wagugunaji ambao wanakamata katika vishimo. Labda hula mayai pia.

Nyoka hawa hawana sumu na huyaua mawindo kwa kuwabamiza dhidi ya ukuta wa kishimo. Wakitishwa huachama mdomo ili kuonyesha rangi ya nyeusi. Kisha huinua kichwa juu na wanaweza kushambulia pia, lakini hawang'ati.

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka mdomo-kulabu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.