Nenda kwa yaliyomo

Nyakatu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyakatu
Nyakatu wa Peters (Leptotyphlops scutifrons)
Nyakatu wa Peters (Leptotyphlops scutifrons)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli: Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda: Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda: Serpentes (Nyoka)
Familia: Leptotyphlopidae
Stejneger, 1892
Ngazi za chini

Nusufamilia 2:

Nyakatu ni nyoka wasio na macho wala sumu wa familia Leptotyphlopidae. Kwa lugha nyingine huitwa “nyoka-nyungunyungu” mara nyingi, kwa sababu wengi wanafanana na nyungunyungu warefu. Wanafanana pia na birisi lakini hawa ni warefu kwa kulinganisha na mkia wa nyakatu ni sehemu kubwa ya mwili kuliko ule wa birisi (10-12% badala na 1-3%).

Nyoka hawa ni wafupi na wembamba, sm 46 kwa kipeo lakini sm 10-30 kwa kawaida. Wana mkia mrefu kiasi. Macho yao yamepunguka mpaka madoa meusi chini ya gamba yanayoweza kulinganua nuru na giza tu. Rangi yao ni nyeusi, kijivu, kahawia au pinki. Rangi hiyo ya mwisho inaonekana wakati ngozi ni kavu.

Nyakatu huchimba ardhini na kuingia vishimo. Kwa sababu ya hiyo hawahitaji macho. Hula wadudu wanaoishi chini ya ardhi, kama vile mchwa, lava wa sisimizi na viroboto. Pengine hupatikana katika viota vya ndege ambapo hula viroboto wa ndege.

Nyoka hawa hawana sumu na kwa kisa chochote mdomo wao ni mdogo sana; kwa hivyo hawawezi kung'ata mtu na wanaweza kukamatwa bila shida.

Spishi za Afrika

[hariri | hariri chanzo]
  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyakatu kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.