Nenda kwa yaliyomo

Norodom Sihamoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Norodom Sihamoni (kwa Kikhmer: នរោត្តម សីហមុនី; amezaliwa 14 Mei 1953) ni Mfalme wa Kamboja[1]. Alipata kuwa Mfalme mnamo 14 Oktoba 2004, wiki moja baada ya kujiuzulu kwa baba yake, Norodom Sihanouk.

Yeye ndiye mtoto mkubwa wa Mfalme Sihanouk na Malkia Norodom Monineath. Alikuwa balozi wa Kamboj a kwa UNESCO. Aliteuliwa na baraza la kifalme kumfuata babake Norodom Sihanouk wakati huyu alipojiuzulu mnamo 2004.

Sihamoni alisoma shule na chuo cha dansi huko Chekoslovakia na alijulikana kwa kazi yake kama balozi wa kitamaduni huko Ulaya na kama mwalimu wa dansi. Yeye hajaoa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Norodom Sihamoni kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.