Nenda kwa yaliyomo

Nikita Krushchov

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nikita Khrushchov)
Krushchov na Stalin 1936
Krushchov na rais Kennedy wa Marekani 1961

Nikita Sergeyevich Krushchov (Kirusi: Ники́та Серге́евич Хрущёв - Nikita Sergeyevich Khrushchyov) (17 Aprili 189411 Septemba 1971) alikuwa kiongozi wa Umoja wa Kisovyeti baada ya kifo cha Joseph Stalin. Alitawala kati ya 1953 hadi 1964.

Krushchov alizaliwa mjini Kalinovka, Urusi. Baadaye alihamia Ukraine. Alikuwa mfanyakazi wa migofi akajiunga na chama cha Bolsheviki.

Alipanda ngazi chini ya Stalin. Baada ya kifo chake akawa kiongozi aliyemfuata. Cheo chake kilikuwa "Mwenyekiti wa chama cha kikomunisti cha Umoja wa Kisovyeti" lakini alikuwa na madaraka kumshinda aliyekuwa na cheo cha rais wa nchi.

Mwaka wa 1964 aliondolewa madarakani na mfuasi wake Leonid Brezhnev.

Kufichua maovu ya Stalin

[hariri | hariri chanzo]

Alipokuwa kiongozi alianza kufichua maovu yaliyotendewa chini ya utawala wa Stalin. Aliondoa sanamu na picha za Stalin kote Urusi na katika nchi zilizokuwa chini ya Urusi. Aliondoa maiti ya Stalin kwenye kaburi alipoonyeshwa kando la maiti ya Lenin.

Mashindano na Marekani

[hariri | hariri chanzo]

Alitangaza shabaha ya kupita kiwango cha maendeleo ya Marekani lakini hakufaulu. Alijaribu kupeleka silaha za nyuklia katika Kuba lakini aliacha mipango hii alipoona kuna hatari ya vita.


Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nikita Krushchov kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.