Nas
Nas | |
---|---|
Nas, akiwa mjini Paris, mnamo 2014
| |
Maelezo ya awali | |
Jina la kuzaliwa | Nasir Jones |
Pia anajulikana kama | Nasty Nas |
Amezaliwa | 14 Septemba 1973 |
Asili yake | Queensbridge, New York City, New York, Marekani |
Aina ya muziki | Hip hop |
Kazi yake | Rapa Mtunzi wa Nyimbo Mtayarishaji wa rekodi Mwigizaji |
Ala | Sauti |
Studio | Ill Will/Columbia The Jones Experience/Def Jam |
Ame/Wameshirikiana na | Weside Connection AZ Bravehearts Nashawn Kelis Foxy Brown Chrisette Michele Nature Jay-Z Kanye West The Game Rakim Busta Rhymes Salaam Remi L.E.S. Large Professor, DJ Premier Dr. Dre Lauryn Hill |
Tovuti | Nas.Defjam.com |
Nasir Jones (amezaliwa 14 Septemba 1973) ni mwanamuziki wa rap na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake kisanii kama Nas. Zamani alikuwa akijiita Nasty Nas. Nas ni mtoto wa mwanamuziki wa jazz wa zamani Mzee Olu Dara. Alizaliwa na kukulia katika nyumba za miradi za mjini (nyumba za watu wenye kipato cha chini) Queensbridge, New York.
Nas alisaini mkataba na studio ya Columbia Records mnamo mwaka wa 1994, na kutoa albamu yake ya kwanza ya Illmatic. Albamu ya Illmatic ilipata kuwa bora na kufahamika zaidi na mauzo bora.
Baadaye albamu kadhaa za Nas zilifuata. Albamu hizo ni pamoja na It Was Written ya 1996, I Am... and Nastradamus ya 1999, na Stillmatic ya 2001. Nas alikuwa mmoja kati ya wanakundi la muziki wa rap na hip hop - The Firm, ambalo limejumuisha wasanii wengine kama vile AZ, Foxy Brown, na Nature. Ingawa kundi halikufanya kazi nyingi lilifanikiwa kutoa albamu moja ya pamoja.
Kuanzia mwaka 2001 hadi`2005, Nas aliusishwa katika ugomvi mkubwa na rapa mwenziwe Jay-Z. Marapa wote walikuwa wakishambuliana kwa kutumia nyimbo zao.
Wawili hao ugomvi wao ukaja kwisha baada ya kualikwa katika tamasha la muziki la New York City-area hip-hop za vituo vya redio. Nas akasaini mkataba na studio ya Jay-Z maarufu kama Def Jam mnamo mwaka 2006.
Albamu yake ya kwanza akiwa kama mmoja wa Def Jam, ilitoka mwaka wa 2006, ikiwa na jina la Hip Hop is Dead, ikiwa imeambatana na albamu nyingine ya mwaka wa 2008, iliyokwenda kwa jina la Untitled.[1]
Muziki
[hariri | hariri chanzo]Albamu za muziki
[hariri | hariri chanzo]- 1994: Illmatic
- 1996: It Was Written
- 1999: I Am…
- 1999: Nastradamus
- 2001: Stillmatic
- 2002: God's Son
- 2004: Street's Disciple
- 2006: Hip Hop Is Dead
- 2008: Untitled
Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina la filamu | Jina alilotumia |
---|---|---|
2001 | Sacred Is The Flesh | kacheza kama "Isa Paige" |
Ticker | kacheza kama "Det. Art "Fuzzy" Rice" | |
1999 | In Too Deep | Alicheza kama Mwuza Madawa Kulevya katika Kona za Mtaa |
1998 | Belly | kacheza kama "Sincere" |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "SoundCircuit.com: Artists: Tributes: Nas". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-03-03. Iliwekwa mnamo 2006-09-06.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- nas.defjam.com Ilihifadhiwa 23 Agosti 2008 kwenye Wayback Machine.
- Nas katika MySpace
- Nas at the Internet Movie Database