Nenda kwa yaliyomo

Namwali Serpell

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Namwali Serpell

Amezaliwa 1980
Nchi Zambia na Marekani
Kazi yake Mwandishi; Mhadhiri

Carla Namwali Serpell (amezaliwa Lusaka, Zambia, 1980) ni mwandishi wa Zambia na Marekani ambaye anafundisha fasihi nchini Marekani. Hadithi fupi na riwaya zake zilipata tuzo za fasihi mbalimbali.

Maisha, elimu, na kufundisha

[hariri | hariri chanzo]

Serpell, baba yake ni profesa wa saikolojia katika Chuo Kikuu cha Zambia na mama yake alikuwa mtaalam wa uchumi ambaye alifanya kazi katika Umoja wa Mataifa.[1]

Serpell na familia yake walihama Zambia mpaka mjini Baltimore, jimbo la Maryland, nchini Marekani, Serpell alipokuwa na miaka tisa.[2] Serpell alisoma fasihi katika vyuo vikuu vya Harvard na Yale.[3] Yeye alifundisha Chuo Kikuu cha California Berkeley kutoka mwaka 2008 mpaka 2020.[4] Sasa yeye ni profesa wa fasihi katika Chuo Kikuu cha Harvard.[5]

Serpell alipata uraia wa Marekani mwaka 2017.[6] Ingawa yeye anaishi Marekani, yeye huenda Zambia kila mwaka.[7] Serpell alisema kwamba nchi zote mbili Zambia na Marekani zina muhimu sana kwake.[8]

Serpell anasema kwamba yeye ni mtetezi wa nadharia ya haki na usawa kwa wanawake.[9]

Maandishi na Tuzo

[hariri | hariri chanzo]

Hadithi, riwaya, na maandishi ya kitaaluma ya Serpell ni kuhusu uhusiano kati ya fasihi na maadili.[10]

Hadithi fupi yake “The Sack” ( “Gunia”) ilipata tuzo ya Caine ya maandishi ya Kiafrika. Serpell aligawana pesa ya tuzo hii na wateule wengine. Yeye aliueleza uamuzi huu aliposema kwamba fasihi si mchezo wa ushindani.[11] Serpell alikuwa mshindi wa kwanza wa tuzo ya Caine ambaye ametoka Zambia.[12]

Riwaya ya kwanza ya Serpell inayoitwa The Old Drift ilichapishwa 2019. Riwaya hii ilipata tuzo za fasihi mbalimbali kama tuzo ya riwaya za sayansi ya Arthur C. Clarke, tuzo kuu ya riwaya za sayansi ya Uingereza.[13] Serpell alijua kwamba yeye aliipata tuzo hii baada ya kusikia kwamba mapolisi ambao walimuua Breonna Taylor hawakushitakiwa kwa mauaji. Kwa hivyo, Serpell aliwapa wapinzani dhidi ya unyanyasaji wa polisi pesa za tuzo yake kama pesa za dhamana.[14]

The Old Drift ni kuhusu familia tatu ambazo zinaishi katika Zambia kutoka wakati wa koloni mpaka wakati ujao karibuni. Waandishi maarufu wa fasihi ya baada ya koloni kama Salman Rushdie na Jennifer Makumbi waliisifu riwaya hii.[15]

Mnamo Machi 2020 Serpell na waandishi saba wengine walipata tuzo ya fasihi Windham-Campbell. Pesa ya tuzo hii ni dala 165,000. Ni moja ya tuzo kubwa za fasihi.[16]

Riwaya ya pili ya Serpell inayoitwa The Furrows ilichapishwa 2022. Riwaya hii inatukia nchini Marekani. Ni kuhusu huzuni ya mwanamke ambaye kaka yake alifariki.[17] The Furrows ilikuwa orodhani kwa rais wa awali wa Marekani Barack Obama kwa riwaya za mwaka 2022 ambazo anazipendelea.[18]

Mchapishaji wa riwaya mbili za Serpell ni Hogarth, sehemu ya Penguin-Random House.[19][20]

  1. https://www.cnn.com/2015/07/08/africa/namwali-serpell-caine-prize-winner/
  2. Sophie Eastaugh (2015-07-08). "5 things you need to know about Caine Prize winner Namwali Serpell". CNN (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  3. Sophie Eastaugh (2015-07-08). "5 things you need to know about Caine Prize winner Namwali Serpell". CNN (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  4. "About". Namwali Serpell (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  5. https://www.namwaliserpell.com/about
  6. https://wheelercolumn.berkeley.edu/2020/05/01/the-zambian-american-perspective-an-interview-with-namwali-serpell/
  7. https://www.npr.org/sections/thetwo-way/2015/07/08/421134703/caine-prize-winner-literature-is-not-a-competitive-sport
  8. https://wheelercolumn.berkeley.edu/2020/05/01/the-zambian-american-perspective-an-interview-with-namwali-serpell/
  9. https://wheelercolumn.berkeley.edu/2020/05/01/the-zambian-american-perspective-an-interview-with-namwali-serpell/
  10. https://books.google.com/books?id=VMyGCgAAQBAJ&pg=PA161#v=onepage&q&f=false
  11. https://www.npr.org/sections/thetwo-way/2015/07/08/421134703/caine-prize-winner-literature-is-not-a-competitive-sport
  12. Flood, Alison (2015-07-07), "Caine prize goes to Zambian Namwali Serpell", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2023-04-25
  13. "About". Namwali Serpell (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  14. "Namwali Serpell Donates Award Money to Bail Funds for Protestors". brittlepaper.com. Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  15. "Namwali Serpell". Namwali Serpell (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  16. "Namwali Serpell Donates Award Money to Bail Funds for Protestors". brittlepaper.com. Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  17. Tope Folarin (2022-10-27). "A World Where Death Isn't the End". The Atlantic (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  18. "Namwali Serpell". Namwali Serpell (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  19. "Hogarth Books | Random House Group" (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-25.
  20. https://www.randomhousebooks.com/books/537834/HG/