Nabii Oded

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nabii Oded (jina la Kiebrania עוֹדֵד, ‘Ōḏêḏ; alizaliwa karne ya 8 KK) alikuwa nabii wa Israeli ya Kale ambaye habari zake zinapatikana katika Kitabu cha Pili cha Mambo ya Nyakati sura ya 28.

Humo tunasoma kwamba, wakati wa mfalme Ahazi, mtu huyo wa Samaria, alikwenda kukutana na jeshi la ufalme wa Israeli likirudi na mateka wengi baada ya kushinda watu wa Yuda vitani akadai warudishwe kwao salama. Kwa kuungwa mkono na viongozi mbalimbali, alifaulu kuwafanya washindi wawatendee kwa wema hao mateka na kuwafikisha Yeriko[1][2].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. M. A. Macleod, "Oded," in The New Bible Dictionary, p. 905.
  2. "2 Chronicles 28:8-15 NRSV - - Bible Gateway". 
Makala hii kuhusu mtu wa Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nabii Oded kama habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.