Mwinyi Chamosi bin Matumula
Mandhari
Mwinyi Chamosi bin Matumula (Matumula) alikuwa mfanyabiashara, mpepelezi na mtaalamu wa lugha aliyeishi Zanzibar katika karne ya 19.
Pamoja na Tippu Tip, alisababisha mageuzi makubwa ya kijamii kwenye bara la Tanganyika hadi Kongo kupitia uwindaji wa tembo kwa minajili ya biashara.[1][2]
Kupitia ubia wake pamoja na chama cha Belgian International African Association, alijichukulia ardhi mashariki kwa Ziwa Tanganyika.
Aliweza kutawala kwa kutumia Warugaruga wake kudai kodi kutoka Mtemi Mirambo wa Wanyamwezi. Ingawa Mirambo alikuwa na jeshi kubwa zaidi, Matumula aliweza kumdai kodi kupitia ulaghai.
Kutokana na hali aliyoisababisha, kipindi cha Vita Ndogondogo kilitokea eneo hilo kati ya miaka 1860 na 1898.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Historia na Utamaduni wa Wapimbe - Peter Mgawe
- ↑ "Guest Bk Volume 2". www.zanzibarhistory.org. Iliwekwa mnamo 2019-08-31.