Mwangati
Mandhari
(Elekezwa kutoka Mwarambe)
Mwangati (Terminalia spp.) | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Mwangati au mpululu
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Miangati ni spishi mbalimbali za mti katika jenasi Terminalia ambazo zina majani madogo kuliko mkungu (Terminalia catappa). Inatokea savana na misitu ya Afrika ya tropiki. Spishi kadhaa, k.m. T. mantaly, hupandwa katika bustani na kandokando ya mitaa. Majina mengine ni mbombaro, mkaa, mkulungo, mpululu, mwalambe, mwarambe na mwavuli. Jina mwangati hutumika pia kwa mti mwingine, Juniperus procera, unaoitwa mtarakwa vilevile.
Spishi za Afrika ya Mashariki
[hariri | hariri chanzo]- Terminalia brevipes, Mwangati
- Terminalia brownii, Mbarao
- Terminalia mantaly, Mwavuli (Madagascar almond)
- Terminalia polycarpa, Mwangati
- Terminalia prunioides, Mwarambe (Purple pod terminalia)
- Terminalia sambesiaca, Mbombaro (River terminalia)
- Terminalia sericea, Mpululu (Silver cluster-leaf)
- Terminalia spinosa, Mwangati (Spiny terminalia)