Mustafa Jaffer Sabodo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mustafa Jaffer Sabodo (14 Mei 1942 [1] – 23 Machi 2024) alikuwa mwanauchumi, mshauri wa masuala ya kimataifa ya ufadhili wa madeni, na mfanyabiashara kutoka nchini Tanzania. Alikuwa na maslahi ya kibiashara nchini India, Ufaransa, Kenya, Sudan, Nigeria, na Zimbabwe.

Maisha na kazi[hariri | hariri chanzo]

Mustafa Jaffer Sabodo alizaliwa Lindi, Tanganyika (sasa Tanzania bara) kwa wazazi wenye asili ya Uhindi.

Mwaka 2003, alijitolea kufadhili ukuaji wa msukumo kwa ajili ya kuuza nje kwa kiasi cha TSh. 100 milioni. [2]

Bahati Nasibu ya Taifa Mwalimu Nyerere Foundation ndiyo iliyoibuliwa na Sabodo, ambaye alitoa TSh 800 milioni kuelekea mradi ulioanzisha bahati nasibu hiyo. [3]

Sabodo alifariki tarehe 23 Machi 2024, Masaki, jijini Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 81. [4]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]