Nenda kwa yaliyomo

Vasektomia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mtumiaji:Lucas559/Vasektomi)
Vasektomia
Mchoro wa anatomia wa vasektomia
Mandharinyuma
Aina ya udhibiti wa kuzaaKufunga kizazi
Matumizi ya kwanzamwaka wa 1899[1]
Kushindwa vya mimba (mwaka wa kwanza)
Matumizi kamili0.10%%
Matumizi ya kawaida0.15%%
Matumizi
Athari ya mudaYa kudumu[2]
UgeuzajiMara chache[2]
Vikumbusho vya mtumiajiUchunguzi wa manii baada ya miezi 3 ili kuthibitisha ufanisi[2]
Manufaa na hasara
Ulinzi kutokana na magonjwa ya zinaa (STD)Hakuna[3]
ManufaaInahitaji tu sindano ya kutia ganzi panapohusika.[2] Ni ya gharama ya chini na salama zaidi kuliko kufunga mirija ya uzazi (tubal ligation).[4][3]
VihatarishiHematoma, maambukizo, maumivu ya muda mrefu[2]

Vasektomia (kutoka Kiingereza: Vasectomy) ni utaratibu wa upasuaji wa kufunga kizazi kwa wanaume.[2] Angalau miezi 3 na kumwaga manii mara 20 kwa ujumla inahitajika ili kufanikisha, jambo ambalo linapaswa kuthibitishwa kwa uchunguzi wa manii.[2] Viwango vya kutofaulu katika hatua hii ni takriban moja kati ya 2,000.[2] Hii kwa ujumla ni njia ya kudumu ya kupanga uzazi kwa sababu inamfanya mtu asiweze kuzaa tena; ingawa kuna njia za kurejesha hali ya kawaida yaani kurejesha uzazi wa kiume, si rahisi, na kuna mbinu ya kuchukua mapema manii ili kutunga baadaye mimba nje ya mwili (in vitro fertilization).[2]

Kwa sababu hiyo inashauriwa kuzingatia kwamba matokeo hayo ya kudumu yanaweza kuathiri saikolojia ya mhusika. Kwa namna ya pekee upasuaji huo haushauriwi kwa vijana wasio na watoto kwa sababu uwezekano wa kughairi baadaye ni mkubwa zaidi, wakija kutamani mtoto na kutambua haiwezekani. Vasektomia ikifanywa bila ujuzi au kibali cha mhusika inahesabika kuwa sawa na kuhasi kwa shuruti.

Ingawa kwa ujumla upasuaji huo ni rahisi na salama upande wa mwili, madhara katika asilimia 1 hadi 2 yanaweza kujumuisha hematoma au maambukizo.[2] Ugonjwa wa maumivu ya baada ya upasuaji huo unaweza kutokea kwa hadi asilimia 6.[2] Utaratibu huu hauathiri uwezo wa kushiriki ngono.[3] Utaratibu huu kwa ujumla unahusisha kutoa kipande cha kila Vas deferens na kuziba ncha zao, jambo ambalo huzuia manii kuingia kwenye uume na hivyo basi kuzuia utungisho.[2]

Upasuaji huo mara nyingi hufanyika katika ofisi ya daktari yenye joto.[2][3] Krimu ya kutia ganzi inaweza kutumika kabla ya kuchomwa sindano ya kutia ganzi.[2] Nywele huondolewa na eneo hilo kusafishwa.[2] Kisha Vas deferens huletwa karibu na ngozi kwenye sehemu ya katikati kati ya korodani na uume.[2] Ili kufikia Vas deferens, ngozi ya juu inaweza kukatwa kwa kutumia kisu cha upasuaji au kufunguliwa kwa kutumia vibano vya upasuaji (forceps) katika mbinu ya kutokutumia kisu cha upasuaji.[2] Kisha sehemu katika Vas deferens huondolewa, hufungwa kwa klipu au kufungwa kwa uzi na kuchomwa..[2] Paracetamol (acetaminophen) na dawa za kuzuia mwasho (NSAIDs) zinaweza kuchukuliwa kwa ajili ya kutuliza maumivu.[2] Kunyanyua vitu vizito sana na kushiriki ngono hakupendekezwi kwa muda wa wiki moja baada ya upasuaji.[2][3]

Upasuaji huu ulifanywa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1899 na Reginald Harrison.[1][5] Kufikia mwaka wa 2020, unatumiwa na wanawake milioni 17 (1.8) wenye umri wa kuzaa kama njia ya kupanga uzazi.[6] Hili ni punguzo kutoka asilimia 6 mwaka wa 1995.[6]

Nchini Marekani, upasuaji huo kwa kawaida hugharimu chini ya dola 1,000 kufikia mwaka wa 2021; [2] ambayo ni gharama ya chini kidogo ikilinganishwa na kufunga mirija ya uzazi (tubal ligation).[4]

  1. 1.0 1.1 Newton, David E. (2 Desemba 2019). Birth Control: A Reference Handbook (kwa Kiingereza). Bloomsbury Publishing USA. uk. PT148. ISBN 979-8-216-05405-4. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 25 Machi 2024.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 2.14 2.15 2.16 2.17 2.18 2.19 2.20 Zeitler, M; Rayala, B (Desemba 2021). "Outpatient Vasectomy: Safe, Reliable, and Cost-effective". Primary care. 48 (4): 613–625. doi:10.1016/j.pop.2021.08.001. PMID 34752273.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Fainberg, J; Kashanian, JA (19 Juni 2018). "Vasectomy". JAMA. 319 (23): 2450. doi:10.1001/jama.2018.6514. PMID 29922830.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. 4.0 4.1 Stormont, G; Deibert, CM (Januari 2024). "Vasectomy". StatPearls. PMID 31751094.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Ciment, James (4 Machi 2015). Social Issues in America: An Encyclopedia (kwa Kiingereza). Routledge. uk. 4. ISBN 978-1-317-45971-2. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Machi 2024. Iliwekwa mnamo 25 Machi 2024.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. 6.0 6.1 World Family Planning 2022 (PDF). United Nations. 2022. ISBN 9789211483765. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo (PDF) mnamo 7 Desemba 2023. Iliwekwa mnamo 22 Machi 2024.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)