Utungisho
Mandhari
Utungisho (kwa Kiingerezaː Fertilisation au fertilization; pia generative fertilisation, conception, fecundation, syngamy na impregnation[1]) ni muungano wa gameti ya kiume na ya kike ambao ni mwanzo wa kiumbehai mpya.
Utungisho ni wakati muafaka katika mchakato mzima wa kuzaliana. Huanza pale mbegu ya manii inapokutana na sehemu ya nje ya kijiyai (ovum) na humalizikia pale kiini cha mbegu hiyo kinapoungana na kile cha yai kuaunda seli moja ambayo baadaye hukua na kufikia hali ya kiumbe kikubwa cha spishi yake.
Utungisho hutokea kwa wanyama hali kadhalika kwa mimea ambayo huzaliana kwa ogani zote za kike na kiume kuchangia katika kutengeneza kiumbe kipya.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Utungisho kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |