Mswati III wa Uswazi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mswati III)
Mfalme Mswati III mnamo mwaka 2014.
Kundi la wake wa Mswati wakikutana na mgeni rasmi kutoka Japani.

Mswati III (amezaliwa 19 Aprili 1968[1]) ni mfalme wa Eswatini tangu tarehe 25 Aprili 1986.

Alizaliwa Manzini kama mtoto wa mfalme Sobhuza II na mmoja wa wake zake wadogo, Ntfombi Tfwala.[2]

Alipokea ufalme tarehe 25 April 1986 akiwa na umri wa miaka 18. Wakati ule alikuwa mfalme mwenye umri mdogo zaidi duniani. Anatawala pamoja na mama yake Ntfombi Tfwala, ambaye sasa ni Mama wa Mfalme (Ndlovukati), akitawala kama mfalme mwenye mamlaka kubwa ndani ya katiba ya ufalme.

Mswati III ni maarufu kwa kuendeleza mila ya kuwa na wake wengi ambao mwaka 2020 walikuwa 15.[3]

Siasa zake, pamoja na maisha yake tajiri katika nchi maskini imesababisha upinzani ndani ya Eswatini na ukosoaji wa kimataifa.[4]

Marejeo

  1. Genealogy:SWAZILAND Archived 19 Mei 2018 at the Wayback Machine, World of Royalty
  2. King Mswati III is born | South African History Online. Sahistory.org.za (1968-04-19).
  3. Laing, Aislinn. "King of Swaziland chooses teenager as 15th wife", The Telegraph, 18 September 2013. 
  4. Bearak, Barry. "In Destitute Swaziland, Leader Lives Royally," New York Times. 6 September 2008.
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mswati III wa Uswazi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.