Mstafeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mstafeli
(Annona muricata)
Mstafeli
Mstafeli
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Magnoliids (Mimea ambayo maua yao yana mizingo ya tepali tatu na chavua yenye kitundu kimoja)
Oda: Magnoliales (Mimea kama mparachichi)
Familia: Annonaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mkonokono)
Jenasi: Annona
Spishi: A. muricata
L.

Mstafeli ni mti mdogo wa familia Annonaceae. Matunda yake yanayolika huitwa mastafeli. Mti huu una maua madogo ya rangi ya njanokijani yenye petali nene. Matunda yana umbo wa yai au figo na rangi ya majani na yana miiba myororo. Nyama ni nyeupe yenye ladha tamu na chachu. Mbegu zake ni nyeusi na kubwa kiasi.

Picha[hariri | hariri chanzo]