Morotonga

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Morotonga ni kata ya Wilaya ya Serengeti katika Mkoa wa Mara, Tanzania yenye postikodi namba 31605[1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 4,108 waishio humo. [2]

Kabla ya kuwa kata, Morotonga kilikuwa kijiji chenye maendeleo makubwa kati ya vijiji vinavyozunguka mji wa Mugumu; kutokana na maendeleo hayo Morotonga ilivutia watu kutoka sehemu mbalimbali, hasa wageni ambao waliwahi kuja na kuishi Mugumu mjini, kupenda kuishi aidha katika nyumba za kupanga na wengine kuomba kuweka makazi yao ya kudumu katika kijiji cha Morotonga. Hayo yote yaliwezekana kutokana na historia na tabia nzuri ya wenyeji wa Morotonga ambao ni Waikoma. Hii pia ni kwa sababu katika kijiji cha Morotonga waliishi watu wastaarabu sana.

Familia za Waikoma zimegawanyika katika milango minane (Bhehita 8).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Serengeti - Mkoa wa Mara - Tanzania

Busawe | Geitasamo | Ikoma | Issenye | Kebanchabancha | Kenyamonta | Kisaka | Kisangura | Kyambahi | Machochwe | Magange | Majimoto | Manchira | Matare | Mbalibali | Morotonga | Mosongo | Mugumu | Nagusi | Natta | Nyamatare | Nyambureti | Nyamoko | Nyansurura | Rigicha | Ring'wani | Rung'abure | Sedeco | Stendi Kuu | Uwanja wa Ndege


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mara bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Morotonga kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.

Usiingize majina ya viongozi au maafisa wa sasa maana wanabadilika haraka mno.