Nenda kwa yaliyomo

Moody Awori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Arthur Moody Awori

Arthur Moody Awori (anajulikana kama "Uncle Moody", alizaliwa Butere.[1][2], 5 Desemba 1927) alikuwa Makamu wa Rais wa 9 wa Kenya kutoka tarehe 25 Septemba 2003 [1] hadi 9 Januari 2008[3].

Awori alikwenda shule ya upili ya Mangu mwaka 1935, na baadaye alisomea Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda.

Alichaguliwa kama Mbunge wa Funyula Constituency katika Wilaya ya Busia katika Mkoa wa Magharibi mwaka 1983.[1][4] Chini ya Rais Daniel arap Moi, alitumikia katika nafasi kadhaa kama naibu waziri.[1][4]

Awori aliachana na chama tawala, KANU, mwaka 2002 na kujiunga na chama cha upinzani cha National Rainbow Coalition na ni mwenyekiti wa kiungo cha juu cha maamuzi cha NARC.[1] Wakati Moi alifanikiwa na Mwai Kibaki, Awori alifanywa Waziri wa 'Home Affairs' Januari 2003 [4] na kisha Makamu wa Rais (kama bado ni waziri) mwezi Septemba 2003, kufuatia kifo cha aliyetangulia Makamu wa Rais, Michael Wamalwa Kijana jijini London.[1]

Awori ni makamu wa rais wa tisa tangu uhuru wa Kenya mwaka 1963. Wengine kabla yake walikuwa Jaramogi Oginga Odinga, Joseph Murumbi, aliyekuwa Rais Daniel arap Moi, sasa Rais Mwai Kibaki, Prof Josephat Karanja, Prof George Saitoti, na Musalia Mudavadi.

Katika uchaguzi mkuu wa Desemba 2007, alipoteza kiti chake Bungeni.[5][6] Tarehe 8 Januari 2008, Kibaki alimpa Kalonzo Musyoka nafasi ya Makamu wa Rais na Waziri wa 'Home Affairs',[6] Awori alipeana ofisi 9 Januari. Awori, alimsema Musyoka kama "rafiki na mwana wa kisiasa", alisema kwamba aliamini Musyoka alikuwa "sawa na kazi", Musyoka naye alisema kwamba alikuwa na "heshima kuu" kwa Awori, aliyemwita "mwanaume kweli".[3]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Mcha Mungu halisi wa Kanisa Katoliki [1], Awori amemuoa Rose Awori. Wana watoto watano wazima - wa kiume wawili na mabinti watatu - mbali ya wajukuu.

Kaka yake, WWW Awori, aliwahi kufanya kazi katika Legislative Council katika miaka ya 1950. Mdogo wake Aggrey Awori ni mwanasiasa nchini Uganda aliyekuja wa tatu katika uchaguzi wa rais wa 2001.[7]

Anglo leasing

[hariri | hariri chanzo]

Amehusishwa katika kashfa ya Anglo leasing katika ripoti iliyochapishwa tarehe 22 Januari 2006 na John Githongo. Alisisitiza kuwa hana hatia na akakataa kujiuzulu kwani hakuona sababu ya kufanya hivyo. Mwezi Februari 2006 Wabunge 80 walidai kujiuzulu kwake, na kutishia maandamano mitaani kama maombi yao hayangefuatiliwa.[8] Siku chache baadaye wapinzani katika mitaa ya Nairobi walitoa mwito wa kujiuzulu kwake kama sehemu ya kupambana na rushwa.[9] Baada ya kutofanikiwa, Kituo cha Mageuzi ya Kijamii kilisema kwamba alikuwa anaudhoofisha uadilifu wa ofisi yake kwa kukataa kujiuzulu na waliahidi kuendelea na maandamano.[10] 22 Februari katika mahojiano na Kamati ya Akaunti za Umma, Awori aliwalaumu watumishi wa umma, akidai wamekuwa wakimpoteza na kwamba alikuwa hana makosa yoyote.[11]

Yeye pia ni mwenyekiti mwanzilishi wa Chama cha Wasiojiweza kimwili cha Kenya, na mwanachama wa Taasisi ya Makatibu.

Yeye ana shahada ya heshima ya udaktari kutoka Chuo Kikuu cha New Hampshire, Amerika. Alituzwa shahada hiyo Mei 2004 kwa kutambua miaka yake mingi ya huduma ya kujitolea kwa jamii, hasa walemavu na maskini.

Katika kutambua mchango wake bora kwa taifa na jamii kwa ujumla, Serikali ya Kenya ilimpa tuzo mbili -Elder of the Burning Spear (EBS) na Elder of the Golden Heart (EGH).

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Alitanguliwa na
Michael Wamalwa Kijana
Makamu wa Rais wa Kenya
2003–2008
Akafuatiwa na
Kalonzo Musyoka