Mona Eltahawy

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
2018 Tuzo za Disobedience katika maabara za MIT

Mona Eltahawy (alizaliwa 1 Agosti 1967) ni mwandishi huru na mchambuzi wa masuala ya kijamii raia wa Misri na Marekani [1], mkazi wa jiji la New York City.

Ameandika makala yaliyochapishwa katika nchi nyingi kuhusiana na Misri na Uislamu, ikijumuishwa masuala ya wanawake , Uislamu na mambo ya siasa pamoja na ya kijamii. Kazi zake zimechapishwa na Washington Post, New York Times, Christian Science Monitor na Miami Herald pamoja na mingine.

Aliandika Headscarves and Hymens kama kitabu chake cha kwanza mwaka 2015. Amealikwa mara nyingi kama mchambuzi katika vipindi vya televisheni na habari nchini Marekani. Anajulikana pia kwa kuanzisha harakati ya Mosque Me Too inayokusanya habari za ubakaji wakati wa safari ya hajj.[2][3][4][5]

Alishawahi kuzungumza kwenye vyuo, mazungumzo ya paneli na kwenye majumuiko ya kiimani kuhusiana na haki za binadamu, matengenezo katika dunia ya Uislamu, haki za wanawake na mahusiano baina Waislamu na Wakristo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mona Eltahawy kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.